Unknown Unknown Author
Title: UCHAMBUZI WA MWANAKIJIJI KUHUSU SUALA LA FROLA MBASHA LINALO ENDELEA AGUSIA MTAZAMO WA JAMII YETU NA UHALISIA KISHERIA;PIA AMEGUSIA SUALA LA IMANI NA MAJARIBU NI VITU VISIVYO EPUKIKA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Mimi Mwanakijiji Wazo la Kijamii: Suala la Flora Mbasha na mme wake lia sehemu nyingi ambazo unaweza kuziangalia na kutolea m...
Wazo la Kijamii: Suala la Flora Mbasha na mme wake lia sehemu nyingi ambazo unaweza kuziangalia na kutolea maoni. Hata hivyo naamini kubwa ni Tatu. Suala la tuhuma za uhalifu - mme wa Flora Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake na pili suala la mahusiano ya kindoa kati ya Flora na Mmewe. La tatu ni suala la kuwa wote wanadai ni Walokole na hivyo kuna hoja ya "ulokole gani huu".

Suala la tuhuma za uhalifu ni rahisi zaidi kulizungumzia. Uhalifu wa ubakaji haujali nani anatuhumiwa kubaka. Sheria haijali kama mtu ni mlokole au mtakatifu, ni tajiri au maskini ni maarufu au siyo. Kwamba binti amedai kuwa amebakwa - kuingiliwa kimwili kinyume na ridhaa yake - ni madai ya suala la uhalifu. Binti anayetendewa hivyo na mtu yeyote anapaswa kushtaki kwa vyombo vya sheria.

Hili si 'kosa' tu la mtu kumkosea mwingine kama ambavyo mazungumzo ya simu ya Mbasha (wa waliobahatika kuyasikia) yanaonesa. Hili ni kosa kubwa sana la kihhisia na kivitendo. Mabinti wengi wanabakwa na watu wa karibu yao; na siri hizi ziko nyingi kwenye familia. Wapo wanaobakwa na baba zao, kaka zao, binamu, marafiki wa ndugu zao n.k Na wapo hata wanaobakwa na wafanyakazi wenzao au mabosi wao na wengi wanajikuta wanalazimika kukaa kimya. Ama kwa vile wanajilaumu wao wenyewe au wanaona kuwa watajidhalilisha zaidi kwa kutokea hadharani.

Alichofanya binti huyu ni kitu cha kutiwa moyo na siyo kukebehewa. Uvaaji wa msichana au uzuri wake au urembo wake siyo uhalalishaji wa udhaifu wa wanaume. Wote tuna udhhaifu wetu na wanaume wengi tumewahi kujaribiwa na wasichana kiasi cha kudhani hatuwezi kujizuia lakini wengi wamejizuia kwa sababu wanafahamu tofauti ya ridhaa na hiari. Hivyo, kwa binti kujitokeza ni suala la ujasiri na uthubutu mkubwa kwani tuhuma hizo bila ya shaka zinaweza kuleta mvurugano (na tayari zimeleta kwenye mahusiano ya Flora na mmewe.

Suala la uhhusiano wa Flora na mmewe ni suala la kwao zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. NI wao wawili waliosimama mbele hadharani na mashahidi wao kuweka ahadi zao za ndoa. Kama wana matatizo ni wao wanatakiwa kwenda kuyatatua na kutafuta ushauri. Kama mmoja wao si mwaminifu kwa mwenzie au wote si waaminifu ni wao wanatakiwa kujipima na kuona kama ahadi zao za ndoa ni kamili. Hakuna ndoa isiyo na majaribu yake, na majaribu yanatofautiana ni vizuri basi watu kujipima wenyewe kuliko kuwalaumu wengine.

Kwenye suala la ulokole kwa kweli kulaani ulokole au walokole kwa sababu ya matendo ya watu wengine ni kutokuelewa mfumo wa utawala wa dhambi. Dhambi haina heshima na haichagui nani wa kumwangusha; alianguka Mfalme Suleiman na alianguka Daudi! Suala kubwa ni je wanaweza kurudi kwenye neema? Je wanaweza kujirudi na kutambua walipoangukia?

Katika ile hadithi y angu inayokuja ambayo inatokana na matukio ya kweli - Upako Kutoka Kuzimu - nimejaribu kudokeza mambo yanayoendelea katika watu wenye imani na ni kwa nini yatupasa mara zote kujitahhidi kurudi kwenye neema bila kujali wapo umeanguka.

Binafsi nawaombea warudi na kutambua huruma ya Mungu. Uhalifu ushughulikiwe hadi kikomo cha sheria bila kujali sura au sifa na hadhi. Nje ya hapo kuna mambo ya kujifunza katika hili lote na ni mafunzo ambayo watu wote walioko kwenye mahusiano - wawe walokole au la - wanapaswa kuyazingatia moyoni.

MMM

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top