Na Hudugu Ng'amilo
Maendeleo
ya sayansi na teknolojia pamoja na kuongezeka kwa mahitaji ya
vifungashio vya bidhaa viwandani, mauzo ya rejareja maduka na kwenye
masoko, kumeongeza matumizi ya mifuko ya plastiki.
Hali hii
imesababisha kuwepo kwa mrundikano kubwa wa taka za plastiki
zinazozalishwa kwenye jamii. Wakati mwingine taka hizi huzagaa katika
maeneo mbalimbali ya vijiji, miji na majiji nchini.
Kutokana
na hali hiyo, mabaki ya taka za plastiki yanazusha changamoto mpya
katika utunzaji wa afya ya jamii na mazingira kutokana na ukweli kuwa
udhibiti wake ni mgumu na haziozi.
Watu
wengi huamua kuchoma taka ngumu ikiwa ni pamoja na mabaki ya plastiki
kama njia rahisi ya kufanya usafi na kudhibiti zisizagae ovyo. Wengine
huchoma mifuko ya plastiki na mabaki mengine kwa ajili ya kuwashia moto
wa matumizi ya nyumbani, mama na baba lishe, migahawa na sehemu
mbalimbali ambazo hutumia mkaa kwa ajili ya kupika.
Daktari
bingwa wa magonjwa ya mfumo wa upumuaji hapa nchini, Dk Meshack Shimwela
anasema kwamba, moshi unaotokana na uchomaji wa mifuko hii ya plastiki
husababisha magonjwa ya mfumo wa upumuaji. Anayaelezea kwamba ni
magonjwa yanayoongoza kwa kuua watu wengi katika nchi maskini duniani.
Taarifa
iliyochapishwa katika gazeti hili la Mwananchi, ukurasa wa 19 toleo la
Juni 6, 2014 inaonyesha uchomaji holela wa plastiki ni moja ya sababu za
uzalishaji wa moshi hatari unaochafua mazingira ya hewa katika nchi
zinazoendelea,Tanzania ikiwa miongoni.
Tafiti
mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa, uchomaji wa plastiki kwa
sababu yoyote ile, husababisha madhara kwa afya ya jamii na mazingira
kutokana na kuzalisha moshi wenye sumu mbalimbali zinazochafua hewa.
Isitoshe
majivu yake yana sumu hatari inayo haribu ubora wa mazingira ya maji,
ardhi, mimea na chakula. Plastiki nyingi zinapochomwa huzalisha sumu
kama vile dioxin, furans, caboni monoksaidi, aldehydes na polynuclear
aromatic hydrocarbons (PAHs).
Hii ni
kwa mujibu wa utafiti wa Valavanidid A. na wenzake uliochapishwa mwaka
2008 katika jarida la malighafi hatari (Journal of Hazardous Materials)
toleo la 156.
Kwa
mujibu wa tafiti nyingi za afya ya jamii na mazingira, sumu hizi
zimeonyesha uwezo mkubwa wa kusababisha saratani na magonjwa sugu ya
mfumo wa upumuaji (OCPD) kama vile pumu, matatizo ya akili, mishipa ya
fahamu pamoja na kushusha kinga ya mwili....(soma GAZET LA MWANANCHI)
MJUMBE Sr
Post a Comment