Unknown Unknown Author
Title: UINGEREZA YAKUMBWA NA UHABA WA MBEGU ZA KIUME
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Uingereza yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume  Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ...

Uingereza yakumbwa na uhaba wa mbegu za kiume
 Uingereza inakabiliwa na upungufu wa Mbegu za kiume hali ambayo huenda ikalazimu kiliniki za matibabu ya uzazi nchini humo kuchukua mbegu duni.
Onyo hili limetolewa na shirika la kijamii la matibabu ya uzazi nchini humo BFS.
 
Inadaiwa kuwa baadhi ya kliniki hizo hutegemea shahawa kutoka nchi za kigeni kutokana na mahitaji yake nchini humo.
Lakini mwenyekiti wa shirika hilo Daktari Allan Pacey amesema kuwa ana wasiwasi kwamba baadhi ya vituo hivyo vya matibabu sasa vinatumia kila njia ili kupata wafadhili wa mbegu hizo.
 
Amesema kuwa wanawake watakabiliwa na mbinu zitakazogharimu kiasi kikubwa cha fedha iwapo mbegu duni zitatumiwa.
 
Inadaiwa kuwa upungufu huo unasababishwa na kuondelewa kwa sheria kwamba majina ya wanaotoa mbegu hizo sasa ni sharti yajulikane ikilinganishwa hapo awali ambapo watu wengi walipendelea kuficha majina yao.
Mahitaji ya wafadhili wa shahawa yanazidi kushuka kwa kuwa maendeleo ya matibabu ya uzazi yanawafanya wanaume wengi kutafuta watoto wao wenyewe.
 
Hata hivyo uhaba wa wafadhili wa mbegu za kiume bado upo.
 
Takwimu kutoka mamlaka ya kudhibti uzazi wa binaadamu zinaonyesha kuwa moja kati ya mbegu nne za kiume zimetoka katika mataifa ya kigeni.
Takwimu hizo zilikuwa moja katika kila mbegu kumi mnamo mwaka 2005.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top