ALICHO SEMA PROF.LIPUMBA;KUHUSIANA NA TAARIFA ZA MHE.SITTA KUTEUA KAMATI YA WATU 27 KWA AJILI YA KUWA RUDISHA UKAWA BUNGENI NA RAI YA MAALIMU SEIF KWA MHE RAIS!!
Prof.Ibrahim Lipumba.
"Msimamo wetu uko wazi tu, kwamba Rasmu ya Katiba iheshimiwe. Bunge la Katiba lina Kazi ya kujadili na kupitisha Rasmu ya Katiba, kwa hiyo ni lazima mjadala uongozwe hivyo, siyo vinginevyo.
"Kiini cha Rasmu ile ni uwapo wa muundo wa Serikali ya Shirikisho, yaani Serikali tatu. Sasa ukienda kwenye Bunge na kuacha mapendekezo hayo na kuleta Serikali mbili, unaitoa wapi?".
Alisema Prof.Lipumba alipokuwa akijibu maswali ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwananchi la leo Tarehe 09/07/2014, kuhusiana na Taarifa za Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Mhe.Samwel Sitta kuteua Kamati ya Watu 27 kwa ajili ya kutafuta mwafaka na maridhiano ya Mchakato wa Katiba mpya.
Maalimu Seif amvaa Kikwete
"Mchakato huu unamtegemea yeye. Hakuna ambaye amekamilika, Rais ajiangalie kama alivyofanya ni sawa, kama sio sawa arekebishe mambo ili kujenga tena imani kwa wadau wote.
"Mfano ni hotuba yake alipokutana na Baraza la vyama vya Siasa ilikuwa nzuri, lakini alipofungua Bunge la Katiba akajisahau kama yeye ni Rais wa Watanzania wote akachukua msimamo wa Chama chake na kuihujumu Tume ya Katiba na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.
"Ushirikiano wa UKAWA utaendelea hata baada ya mchakato wa Katiba kumalizika.
"Hii ni pamoja na kuangalia kama tunaweza kuachiana majimbo ya uchaguzi iwapo Chama kimoja kitaonekana kina nguvu zaidi kuliko kingine katika eneo fulani".
Alisema Maalim Seif.
Tundu Lissu (Mb),
Mjumbe wa Bunge Maalumu
09/07/2014.
Post a Comment