ALICHO ZUNGUMZA DKT SLAA KUHUSU KAULI YA MSAJILI WA VYAMA ILIYO MTAKA KUTOGOMBEA;KWA SABABU HANA SIFA ZA KUGOMBEA TENA UONGOZI WA CHAMA HICHO!
DKT SLAA AAMUA KUTOA YA MOYONI LEO,AMVAA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA,SOMA ALICHOZUNGUMZA NA MTANDAO HUU
Na karol vicent
SIKU moja kupita baada, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kusema Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa hawana sifa za kugombea tena uongozi wa chama hicho kwa kuwa wanabanwa na katiba yao,
Naye ,katibu mkuu wa chama hicho,ameibuka na kusema wao watapuuza kile anachokiita ni njama zinazotumika kukibomoa chama hicho,kwani utaratibu aliotumia aukufuata kanuni yeyote katika maamuzi hayo.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu chama cha Maendeleo CHADEMA, Dk Willibrod Slaa wakati alipokuwa anafanyiwa mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu,kutaka kujua kuhusu kauli ya chadema baada ya maamuzi ya Msajili wa vyama vya kisiasa,ambapo alisema Msajili wa Vyama vya Siasa amefanya maamuzi bila ya kuwasiliana na chama hicho,na maamuzi ya kufanya hivyo ni ishara sasa msajili anatumika kukibomoa chama hicho.
Dk Slaa,aliongeza sababu anayoisema kwamba chama hicho imeondoa kipengele cha ukomo wa uongozi sio kweli,bali katiba ya chadema inahitaji mapendekezo yote ya katiba yaanzia kwenye ngazi za Mabaraza ya wilaya na kupanda hadi kwenye baraza za mikoa.
“Katiba ya chadema inahitaji mapendekezo ya mabadiliko ya katiba yaanzia kwenye mabaraza ya wilaya na kupanda hadi kwenye baraza ya mikoa ya chama pamoja na mabaraza yake yote yani ya Vijana,wazee pamoja na wanawake,na yakitoka mapendekezo hayo mpaka yanafika kwenye mkutano mkuu na kuyatolea maamuzi”alisema Dk Slaa
Mwandishi wa Mtandao huu alipomtaka kutolea ufafanuzi kuhusu kipengele cha ukomo wa Uongozi kilichotolewa kwenye Katiba ya chama hicho.
Dk,Slaa alisema kifungo hicho kilitolewa kuanzia viongozi wa chini na wala sio matakwa ya viongozi wa Juu.
“Kifungu hicho kiliondolewa kutoka chini kwani katiba ilipelekwa huko chini kwenye mabaraza na mapendekezo yalipelekwa chini na kukakubalika na hicho kipengele kilikubalika huko chini na kufika makao makuu yaanza kujadiliwa na sisi ndio tulivyofanya, kumbukeni mkutano mkuu sio kazi yake kutunga katiba kazi yake kupisha yale ambayo vyombo vyake vimefanyiwa kazi”alisema Slaa
Katika hatua nyingine Dk Slaa aliwashangaa watu wanaojiita viongozi wa chama hicho kwa kuanza kuwalalamikia viongozi wa chama,kwani wamekaa kimya kipindi cha miaka kumi kuja kulalamika sahivi.
“Nashangaa hao viongozi wanalalamika,sasa kwanini wasingelalamika huko kwenye kamati za wilaya na kamati za mikoa huko ndio wangelalamika,nashangaa leo wanalalamika baada ya miaka kumi kupita ndio wanaanza kulalamika.”
“Halafu kuna viongozi walimaliza uongozi katika vipindi viwili viwili,kama kipengele hicho kingekuwepo kama Mzee ndesambulo asingechaguliwa 2009, mara ya tatu kutokana na marekebisho katiba kumruhusu pamoja mzee Katisiko Mkoani Kigoma amechaguliwa kutokana na Katiba kumruhusu,wako viongozi wengi ambao wapo kutokana Katiba kumruhusu”alisema Dk Slaa.
Vilevile Dk Slaa,aliwataka wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kupuuzia maelekezo kutoka kwa msajili kwani ushauri wake hakuzingatia katiba ya Chadema na kuwataka kupuuzia kwani unalengo kukivuruga chama hicho.
Asante Habari 24
MJUMBE Sr
Post a Comment