AZAM,YANGA HAZIIBUSISUMBUI MBEYA CITY;MWAMBUSI!
Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema muda wa wiki nne hadi sita unamtosha kuiandaa timu yake kwa ajili ya msimu ujao, hivyo hakuona haja ya kuendelea na mazoezi wakati Ligi Kuu Tanzania Bara imesogezwa mbele.
Timu za Azam, Simba na Yanga zimeendelea na maandalizi yao kwa ajili msimu ujao lakini Mwambusi alisema kila kocha ana programu yake na anafahamu anachokifanya hivyo muda uliopo unamtosha kuandaa timu ya kupambana na vigogo hivyo.
Mwambusi alisema:“Timu nyingine zimekuwa na maandalizi ya muda mrefu ila kwetu hilo si tatizo, nitaiandaa timu kwa wiki nne hadi sita na itakuwa nzuri kwa ajili ya kupambana msimu ujao, huo muda unatosha sana.”
Kwa upande mwingine kocha huyo alisema hana taarifa zozote za kutaka kuondoka kwa mshambuliaji wa timu hiyo, Saady Kipanga na ameshangaa kusikia amefanya mazungumzo na viongozi wa Simba wakati bado ana mkataba na timu hiyo.
“Mchezaji yeyote anayetaka kuondoka aje tu tuzungumze, kikubwa nitakaa na kuzungumza naye kabla ya yeye kuondoka ila si kwamba nitamzuia. Mpaka sasa hakuna mchezaji aliyenifuata ama kunitaarifu kuwa anataka kuondoka hivyo siwezi kuzungumza zaidi juu ya hilo,” alisema Mwambusi
• Mwanaspoti
Post a Comment