Unknown Unknown Author
Title: BAADA YA UVUMI WA TETESI ZA KUWEPO TAARIFA ZA MBEYA CITY KUWA TEMA BAADHI YA WACHEZAJI WAKE;HII NDIYO TAARIFA RASMI ILIYO TOLEWA NA MBEYA CITY!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
MBEYA CITY FC PRESS REALESE NO.03 MCHAKATO WA USAJILI 2014/2015. Kikao cha bodi kilichoketi tarehe 19/6/2014 kiliazimia kuwa klabu imefung...
MBEYA CITY FC PRESS REALESE NO.03 MCHAKATO WA USAJILI 2014/2015. Kikao cha bodi kilichoketi tarehe 19/6/2014 kiliazimia kuwa klabu imefunga rasmi zoezi la usajili kwa msimu ujao wa 2014/2015. Hii ni kutokana na klabu kuwa na mipango ya kupunguza kikosi ili kuwa na kikosi kidogo na chenye ufanisi(tija) na kwa kuzingatia klabu kwa msimu uliomalizika na msimu ujao kutokuuza wachezaji wake. Baadhi ya wachezaji watapandishwa toka katika kikosi cha pili na wachezaji wawili wapya waliojiunga na timu kwa ajili ya msimu ujao 2014/2015 wanatosha. Mchakato unaoendelea toka tarehe 25/6/2014 ni kutafuta wachezaji kwa ajili ya kikosi cha pili (Juniour team) A na A2, mchakato huu utamalizika tarehe 2/7/2014. Lengo ni kupata wachezaji wenye umri kati ya miaka 17-21. Wachezaji ambao muda wao wa kuendelea kuitumikia klabu umefikia tamati ni hawa wafuatao: Aziz Sibo(mkataba umekwisha muda wake 31/5/2014), Mohamed Suleiman(Kapangiwa majukumu mengine), Baraka Haule, Francis Casto, Jeremiah John Mangasini, Richard Brown, Yusuph Wilson(kutolewa kwa mkopo), Geofrey Jackson(kutolewa kwa Mkopo). Watumishi ambao mikataba yao imekwisha muda wake na kwa sababu mbalimbali zinazojulikana kwa pande zote mbili imeshindikana kuihuisha ni Fredy Jackson aliyekuwa Afisa Habari(mkataba wake umekwisha tarehe 31/05/2014) na aliyekuwa Kocha msaidizi Maka Mwalwisi (Mkataba wake umeisha tarehe 30/06/2014). E.E.Kimbe KATIBU MKUU MCC FC 29.06.2014 SOMA ZAIDI........
MBEYA CITY KUINGIA KAMBINI JULAI 15, MWAMBUSI APANIA MAKUBWA ZAIDI MSIMU UJAO LIGI KUU Zikiwa zimebaki siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa, benchi la ufundi la Mbeya City limesema liko katika mikakati mikali ya kusajili wachezaji katika nafasi ya kiungo. Kocha wa Mbeya City, Juma Mwambusi amesema yuko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa viungo wazoefu kabla dirisha la usajili halijafungwa rasmi Julai 15. Mwambusi ambaye ni kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu, amesema kikosi chake hakijaingia kambini Julai 15 kujiandaa kwa msimu ujao wa ligi hiyo. ameelezea mikakati ya Mbeya City msimu ujao "Tumefanya usajili wa safu ya ushambuliaji na sasa tatizo tunalo kwenye safu ya kiungo. Tunao viungo wazuri wa kikosi cha kwanza lakini hatuna viungo wa akiba. Kufikia Julai 14 tutakuwa tumeshapata wachezaji wa nafasi hiyo maana tayari tuko katika mazungumzo ya mwisho na wachezaji hao," amesema Mwambusi huku akibainisha kuwa viungo hao wanatoka ndani ya mipaka ya Tanzania. "Tutaingia kambini rasmi Julai 15 lakini bado sijajua tutaweka kambi yetu maeneo gani maana kuna sehemu tatu ambazo zimependekezwa. Kufikia Julai 14 nitakuwa nimeshachagua mahali pa kwenda," amesema zaidi Mwambusi. Amesema kambi hiyo itakuwa ndani ya mipaka ya Tanzania kwa kuwa klabu hiyo haina utaratibu wa kuweka kambi na kusajili wachezaji wa nje ya nchi. Hata hivyo, kocha huyo hakuwa tayari kuyaweka wazi maeneo ambayo uongozi wa timu hiyo umependekeza kwa ajili ya kambi ya timu yake. Ikiwa chini ya Mwambusi, huku ikishiriki kwa mara ya kwanza VPL, Mbeya City imemaliza nafasi ya tatu msimu huu ikizidiwa kete na mabingwa wapya Azam FC na waliokuwa mabingwa watetezi, Yanga waliokamata nafasi ya pili. Mbeya City tayari imeshamnasa straika hatari Themi Felix kutoka kwa wakatamiwa wa Kagera, Kagera Sugar. • Na Renatus Mahima

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top