Unknown Unknown Author
Title: CHUO KIKUU MZUMBE CAMPUS YA MBEYA CHASAMEHEWA DENI LA BIL2.4 NA JIJI LA MBEYA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, limekubali kusamehe deni la shilingi Bilioni 1.3 kutoka chuo Kikuu cha Mzumber Cumpas y...
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya, limekubali kusamehe deni la shilingi Bilioni 1.3 kutoka chuo Kikuu cha Mzumber Cumpas ya Mbeya. Chuo hicho kilitakiwa kulipa malipo ya shilingi Bilioni 2.4 ya kiwanja namba 8 kitalu G kilichopo eneo la Iwambi kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya kudumu. Taarifa ya kusamehewa dneni hilo limetolewa katika kikao cha Kawaida cha Baraza cha mwisho wa mwaka cha Baraza hilo. Wakizungumza katika kikao hicho , Madiwani hao wamesema baada ya kutambua umuhimu wa chuo hicho ndani ya Jiji la Mbeya kwa kupitia fursa zitakazo patikana hivyo kwa pamoja wameamua kutoa eneo hilo la ardhi ikiwa ni mchango wao. Mmoja wa Madiwani hao Ndugu Lukasi Mwampiki amesema sula la uwepo chuo kikuu hicho ni muhimu kwani kimetoa fursa nyingi za ajira hususani kwa kuajili watumishi wa chuo hicho sanjali na ufanyikaji wa biashara.\ Aidha amefafanua kuwa ,chuo hicho ambacho kwa sasa kimejenga majengo yake katika eneo la Forest lililopo katikati ya Jiji la Mbeya, kimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii licha ya watu kujiendeleza kielimu. Akizungumzia hilo, Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga, amesema kabla ya kufikisha suala hilo kwa Madiwani, uongozi wa halmashauri uliona ni vyema ukajidhihirishia kwa kufanya tathimini mbalimbali kabla ya kukubaliana na ombi hilo. Amesema, uongozi uliunda kamati ambayo ilifanya tathimini juu ya hasara na faida zitakazo patikana kutokana na uwepo wa chuo hicho na kubaini ya kwamba faida ni nyingi hivyo kuruhusu deni hilo kusamehewa. Aidha, akitoa neno la shukrani Mkuu wa chuo cha Mzumbe Cumpasi ya Mbeya, Profesa. Ernest Kihanga, amesema kuwa chuo hicho kinajumla ya wanafunzi 2630 ambapo kwa mwaka wanaichangia serikali zaidi ya milioni 600. Hata hivyo Profesa Kihanga, alitumia nafasi hiyo kulishukuru Baraza la Madiwani la jiji la Mbeya kwa kutambua umuhimu wa chuo hicho na kuamua kusamehe deni hilo. • Na EmanuelMadafa

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top