Diamond Platinumz amelazimika
kubadili ratiba ya kutua katika
uwanja wa ndege wa mwalimu
Julius Nyerere akitokea Marekani
alikoenda kuwakilisha Tanzania
katika tuzo za AFRIMMA na
kushinda tuzo ya mwimbaji bora
wa kiume Afrika Mashariki.
Ambapo mashabiki wake
wanatarajiwa kumpokea.
Mkali huyo wa Bongo Flava
ameiambia 100.5 Times F kuwa
amelazimika kubadili ratiba ya
safari yake kutokana na mabadiliko
ya ndege aliyopaswa kusafiri nayo,
hiyo badala ya kufika leo saa nane
usiku kama alivyokuwa ametaarifu
awali, atafika kesho saa moja
kamili asubuhi.
“Kiukweli Flight yangu ilikuwa
inatakiwa iwepo kuanzia siku ya
leo saa nne. Lakini bahati mbaya
kutokana na matatizo ya ndege
kuingiliana huku na kule
hatujajua…imebidi connection
ziwe nyingi sana. Ilibidi kupelekea
kufika kesho kwenye saa moja
kama na nusu hivi ndio tutakuwa
tunadondoka.
“So, kwanza niombe radhi, najua
watu wengi walikuwa wanataka
kuja lakini bahati mbaya imekuwa
hivyo ni nje ya uwezo wetu. Kama
watu wana nguvunguvu naomba
tukutane pale saa moja asubuhi
mimi ndio nadodondoka.”
Amesema Diamond kwenye
maelezo yake.
Post a Comment