Unknown Unknown Author
Title: INGIA HAPA UZIJUE HAKI ZAKO KAMA RAIA KISHERIA UNAPO KAMATWA NA POLISI! WENGI HATUZIJUI KABISA,BOFYA HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mhe.Tundu Lissu at Dar Es Salaam Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi Raia unayo haki ya:- *Kumwomba Askari ajitambulishe kwako. -...
Mhe.Tundu Lissu at Dar Es Salaam Haki zako za Kisheria unapokamatwa na Polisi Raia unayo haki ya:- *Kumwomba Askari ajitambulishe kwako. -Muulize Jina lake. -Muulize namba yake ya Uaskari. *Kujulishwa ni kwa nini unatiliwa mashaka au kukamatwa. *Kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki ama sehemu unakofanyia kazi kwamba ama umekamatwa na Polisi au TAKUKURU. *Kuomba na Kupewa dhamana wakati ukiwa Kituo cha Polisi ama TAKUKURU. *Hutakiwi kutoa Fedha kama Dhamana uwapo Kituo cha Polisi ama TAKUKURU, isipokuwa maelezo utakayoyatoa na kuandikwa Kituoni hapo. *Kuwaeleza Polisi ama Maafisa wa TAKUKURU kwamba lolote utakalolisema linaweza kutumika kama ushahidi mahakamani na usiburuzwe wakati wa kuyatoa maelezo hayo. *Kuomba wakili wako au mtu wa karibu yako utakayemchagua ili awepo Kituo cha Polisi ama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wakati unatoa maelezo yako. *Haki ya kuyasoma maelezo yako kabla ya kutia sahihi katika maelezo hayo. *Kudai risiti ya Orodha ya vitu vyako/fedha zako ulizotoa ama kukabidhi Kituo cha Polisi ama TAKUKURU. *Haki ya kufikishwa mahakamani katika muda usiozidi Saa 24 tangu alipokamatwa na kufikishwa Kituoni. Haki za Raia Kupekuliwa *Mtuhumiwa anayo haki ya kumpekua Polisi kabla ya yeye kupekuliwa na Polisi huyo. *Raia kama ni Mwanamke, anayo haki ya kupekuliwa na Askari wa Kike, na iwapo Askari wa Kike hayupo, basi Mwanamke yeyote anaweza kumfanyia upekuzi, vile vile kwa Mwanaume. *Askari hawana haki ya kuingia kwenye Gari, Nyumba au Ofisi ya Mtu wanayemtuhumu, kwa madhumuni y kufanya upekuzi bila kuwa na: (a) Hati ya Upekuzi ambayo hutolewa Mahakamani. (b) Mashahidi wanaotambulika rasmi Kisheria, kama vile Mwenyekiti/Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji husika. (c) Jirani wa Mtu anayetuhumiwa. Aidha, Mtuhumiwa hatakamatwa au kupekuliwa na Askari Polisi baada ya Saa 12:30 Jioni au kabla ya Saa 12:30 Alfajiri, kwa mujibu wa makosa ya Jinai (Penal Code Act). Isipokuwa tu, kama kutakuwa na ushahidi wa kutosha kwamba kumpekua Mtuhumiwa kabla ya Saa 12:30 Alfajiri au baada ya Saa 12:30 Jioni kunaweza kuleta madhara kwa Askari Polisi, Mashahidi au Watu wengine wowote wale. Share na marafiki zako!!!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top