Unknown Unknown Author
Title: MHE.JAKAYA KIKWETE AKIWA KWENYE MAHAFALI YA KOZI YA PILI YA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Strateji...
Rais Jakaya Mrisho Kikwete Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
Picha ya Pamoja. PICHA NA IKULU

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top