Siasa ni jambo ambalo limeshikilia
hatma ya vitu vingi sana duniani
ikiwemo mchezo wa soka ambao
una ufuasi mkubwa ulimwenguni
kote.
Nchini Hispania – Raisi wa chama
cha mpira wa miguu nchini
Hispania (LFP) Javier Tebas
amesema kwamba klabu ya FC
Barcelona haitoweza kushiriki
kwenye ligi ya nchi hiyo maarufu
kama La Liga endapo tu kama
jimbo la Catalunya lipata uhuru
kutoka kwa Spain.
Jimbo la Catalunya ambalo lina
miji minne ya Barcelona, Girona ,
Lleida, na Tarragona limekuwa
likipigania uhuru wake kutoka
Hispania kutokana na tofauti zao
na nchi kwenye upane wa
utamaduni na lugha.
FC Barca imekuwa alama ya
harakati hizo za Catalunya lakini
sasa Raisi wa LFP Javier Tebas
amesema kwamba klabu iyo
itashindwa kushiriki kwenye La Liga
kwa sheria na kanuni zilizopo hivi
sasa.
“Sipendi kufikiria suala hilo
kutokea, naamini Catalunya
itaendelea kuwa ndani ya Spain,”
alikaririwa na gazeti la AS.
“Na sina pekee kwa FC Barcelona,
pia vilabu Nastic, Girona, Espanol,
Llagostera na Sabadell. Ikiwa sheria
ya michezo itaendelea kubaki kama
ilivyo, basi watashindwa kushiriki
kwenye ligi yetu.”
Milard ayo.com
Post a Comment