Unknown Unknown Author
Title: SUGU AWAJIBU UVCCM;MBEYA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SUGU AWAPASHA CCM,Dar24 Kufuatia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumshambulia Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHAD...
SUGU AWAPASHA CCM,Dar24 Kufuatia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumshambulia Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), ukimuita mpangaji katika jimbo hilo, amewajibu akisema kuwa wanaota ndoto za mchana. Mbilinyi maarufu kama Sugu, alisema vijana hao hawazijui siasa za jimbo hilo ambapo amewaambia kuwa vijana hao ndio wapangaji, na kwamba wasitarajie mteremko kwani yeyote atakayesimamishwa katika jimbo hilo kupitia CHADEMA ataibuka mshindi kutokana na wananchi wa Mbeya kuendelea kuwa na imani na chama hicho. “Ndugu zangu, Jimbo la Mbeya ni sawa na Mkinga ama Mpemba aliyeenda Kariakoo, amenunua nyumba chakavu akaibomoa na kupandisha ghorofa zaidi ya tatu, halafu aliyeuza nyumba hiyo anaibuka na kusema hao watu ni wapangaji, si atakuwa anachekesha?” amehoji Sugu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top