HII NDIYO KAULI YA JAJI WEREMA ILIYO ZUA UTATA;KUHUSIANA NA MCHAKATO WA BUNGE MAALUM LA KATIBA UNAO ENDELEA,DODOMA!
Pichani ni Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Jaji Fredrick Werema akiwa na Mbunge wa Kigoma kusini David Kafulila Picha na Maktaba.
Na Karoli Vinsent
KILE kinachoonekana Mchakato upatikanaji katiba mpya umeanza kuwachanganya Viongozi wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete,kutokana na wao kuanza kutofautiana kuhusu idadi ya thelusi 2 ya 3 wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Mtandao huu unaripoti.
Mchanganyiko huo umegundulika leo Jijini Dar es Salaam na Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Fredricki Werema wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari alioutisha mahususi ili kuzungumzia kuhusu mchakato wa katiba
Ambapo Werema alisema anahofu juu ya uwezekano wa Katiba mpya kupatikana kutokana na kukosa thelusi 2 ya 3 wajumbe kutoka Zanzibar ambao wengi wao ndio waliogoma kurejea na kujiundia Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA.
“Kuhusu Idadi ya kura za wajumbe wabunge maalum la katiba inatoa wasiwasi kwasababu kwenye Kamati zile thelusi 2 ya 3 ya wajumbe inapatikana bila shida ila tatizo itakuja wakati wakupitisha Rasimu iliyojadiliwa na Bunge ndio itatupa shinda kwasababu lazima ipatikane therusi ya 2 ya 3 kutoka kwa wajumbe wa Tanzania Bara na,”
“ Zanzibar sasa ungiangalia hapa kwa hali ilivyo kama ikiendelea hivi bila ya kuwepo UKAWA itakuwa ni shida kupata Thelusi 2 ya 3 kutoka kwa wajumbe wa Zanzibar na hapa ndio watu wanasema tutakuwa tumetumia pesa nyingi sana za walipa kodi harafu hakuna katiba ndio maana nawaomba ukawa warejee”alisema Werema.
Jaji Werema ambaye naye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba alizidi kusema endepo hali hiyo ikitokea itabidi Bunge la kawaida likae na kuanza kuifanyia marekebisho katiba ya sasa iliyopo hususani kwenye vipengere vinavyopigiwa kelele ikiwemo kuwepo na tume huru ya uchaguzi na sehemu zengine ili kuipa nafasi ya kutafuta Therusi 2 ya 3 kwa wajumbe kutoka Zanzibar.
Kauli ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Werema inazidi kuwachanganya wananchi kutokana na Juzi Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete kusema Katiba mpya itapatikana hata kama Wajumbe wanaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA bila hata kuwepo kutokana na umoja huo kuwa na idadi ndogo sana ya wajumbe.
Ikulu hiyo ilizidi kusema kuhusu idadi iliyopo ya wajumbe kwenye Bunge Maalum la Katiba inatosha sana kuweza kupata idadi ya Therusi 2 ya 3 kwa wajumbe kuweza kuipigia kura vipengere hivyo.
Kauli hiyo pia ilitolewa na Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba Samwel Sitta ambapo alisema katiba mpya itapatikana bila ya UKAWA kuwepo,kwani Idadi ya Wajumbe iliyopo inatosha sana kupata katiba mpya.
Kwa kauli ya Mwanasheria mkuu Jaji Werema inakwenda sambamba na Mwanasheria wa Umoja wa Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA,Tundu Lissu ambapo naye aliuambia mtandao huu kwamba Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete inajisumbua kusema Idadi ya wajumbe wanatosha kupisha rasimu inayojadiliwa na Bunge Maalum na kusema sio kweli,
Kwani idadi iliyopo Bungeni ni ndogo kutokana na Sheria kusema lazima kuwepo na idadi ya 2 ya 3 kutoka kwa wajumbe.
Katika hatua Nyingine Mwanasheria wa Serikali Jaji Werema aliwaomba Wajumbe wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA waliosusia bunge hilo kurejea kwenye bunge hilo kwani wao ni watu muhimu sana .
“Mimi nawaomba ndugu zangu hawa wa Ukawa warejee bungeni kwani mchakato huu unahitaji ushirikiano wao,hebu tuajiulize sote tunaitaji mchango wa Tundu Lissu wakati wa kujadili masuala ya haki za Binadamu tunataka kujua yeye anasemaje lakini kukataa kuja seheme zingine s,nawaomba sana warudi jamani,wengine wajumbe hawa tunasali nao kanisani ikiwemo ndugu yangu Mbatia aje bwana bungeni”alizidi kusema Werema.
Vilevile Jaji Werema alisema kwa sasa Hakuna kipengere chochote cha Sheria kinachompa Mamlaka Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bung la Katiba na kuwataka watu wanasema hivyo waende kusoma sheria.
Post a Comment