Unknown Unknown Author
Title: KUHUSIANA NA EBOLA,CANADA KUTOA CHANJO YA MAJARIBIO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Serikali nchini Canada inasema kuwa itatoa hadi dosi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la afya ulimwenguni...

Serikali nchini Canada inasema kuwa itatoa hadi dosi 1,000 za chanjo ya majaribio ya ugonjwa wa Ebola kwa shirika la afya ulimwenguni WHO.

Hii ni kwa elengo la kusadia kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.

Hatua hii ni baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado infanayiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.
Waziri wa afya nchini canada Rona Ambrose amesema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dosi 500 za dawa hio lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu.
Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kuunda kiwango cha dawa ambacha kinaweza kutumiwa.
Kamapuni moja wa kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio inasema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo.
BBC SWAHILI

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top