Hili ni bango kubwa unalokutana nalo unapoingia geti kuu kuelekea ndani ya viwanja vya maonyesho
Na hii ndio ramani ya eneo zima la maonyesho ya nanenane hapa mkoani mbeya na kumpa mwananchi uelekeo maalumu na sehemu hususa ambazo angependa kutembelea
Nje ya uwanja kulikuwa na magari mengi ya wenyeji na wageni pia kwa ajili ya maonyesho haya makubwa ya kilimo.Kamera ya Mjumbe blog pia ilipata wakati mgumu kutokana na wingi wa watu katika eneo hili
Miongoni mwa mabanda ambayo Mjumbe blog ilitembelea ni Pamoja na Mamlaka ya Jiji la Mbeya kama inavyoonekana pichani.Hapa unapata maelezo Mbalimbali kuhusu Jiji letu la Mbeya.
Hapa ni Banda la Benki ya CRDB ambao pia wanapatikana katika maonyesho haya makubwa ya kilimo
Hili ni eneo la hifadhi za taifa (TANAPA) ambapo wananchi wanapata fursa ya kujionea wanyama wa aina mbalimbali kama vile Simba,chui,Chatu,swala na wanyama wengineo.
Na huu ni moja kati ya vitu ambavyo mwanahabari wetu amepata kujionea,ni mpira uliotengenezwa kwa zao la mpira na kujazwa upepo ndani yake ambao kwa macho na ubora wake unavutia sana
ENDELEA KUTUTEMBELEA ILI UPATE MUENDELEZO WA MAONYESHO HAYA YA NANENANE MKOA WA MBEYA
Post a Comment