Mashuhusda wa tukio hilo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea wakati basi hilo likiwa katika mwendo kasi na kutaka kulipita lori la mafuta lililokuwa liko mbele yake na kusababisha kugongana na daladala hiyo na kupelekea watu watano kufa papo hapo.
Taarifa za awali zinasema kuwa, mara baada ya ajali kutokea dereva wa basi la Hood alijaribu kukimbia lakini wananchi waliweza kumtambua na kumkamata kutokana na sare alizovaa.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kuwa taarifa zaidi itatolewa baada ya kujua idadi ya majeruhi na watu waliopoteza maisha kutokana na baadhi ya majeruhi kuwa na hali mbaya.
Amesema majeruhi wa tukio hilo wamepelekwa katika Hospitali ya mkoa wa huo Mount Meru.
Picha zaidi za tukio hilo hizi hapa
Asante sana Huzwaimata
Post a Comment