Unknown Unknown Author
Title: UMESIKIA KUHUSU DOKTA SLAA KUTAKA KUUWAWA NA MAKADA WA CCM?SOMA HAPA..
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Madiwani walioasi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamerejea na kudai walirubuniwa na makada watano wa CCM kuhama kwenye ...


Madiwani walioasi Chama cha
Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wamerejea na
kudai walirubuniwa na
makada watano wa CCM
kuhama kwenye chama hicho
ili wawatumie kuwaua, Dk.
Willbrod Slaa na John Mnyika.
Helkopta ya Chadema ikitua
katika viwanja vya Shycom
mjini Shinyanga ikiwa
imebeba viongozi wa
Chadema taifa akiwemo Dr
Slaa na John
Mnyika,iliyodaiwa kutaka
kuripuliwa na madiwani wa
chadema mapema mwaka huu-
Picha kutoka Maktaba b
Madiwani hao ni Sebastian
Mzuka wa kata ya Ngokolo na
Zacharia Martin Mfuko wa
kata ya Masekelo wote kutoka
Shinganya mjini ambao
wamewataja makada hao kuwa
ni Naibu wa Waziri wa Fedha,
Mwigulu Nchemba na Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana.
Wengine ni Naibu waziri wa
Nishati na Madini, Steven
Masele ambaye pia ni Mbunge
wa Shinyanga mjini, Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa NEC,
chama tawala, Nape Nnauye,
na Habibu Mchange
(aliyefukuzwa Chadema).
Wakizungumza na waandishi
wa habari jana jijini Dar es
Salaam katika ofisi za chama
hicho, madiwani hao
walisema kuwa, mauaji hayo
yalipangwa kutekelezwa kwa
kiasi cha Sh. milioni 180.
Diwani Mzuka alisema
wamefika kwenye ofisi hizo ili
kueleza kinachoendelea
kudhoofisha chama na kuomba
toba baada ya kuhama.
Alisema mara baada ya
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe kuvuliwa
madaraka Chadema, Mchange
alipewa kazi (dili) na CCM
kutafuta viongozi na madiwani
wa Chadema lengo likiwa ni
kukidhoofisha.
Alisema Mchange aliwafuata
Shinyanga kuzungumza nao
kuhusu suala hilo.
Alisema Januari 27, mwaka
huu alipewa kazi ya kulipua
helkopta iliyokuwa ikitumiwa
na Katibu Mkuu Chadema, Dk.
Slaa, Mbunge wa Ubungo,
Mnyika na Mwenyekiti wa
kanda ya Mashariki katika
ziara ya Kanda ya Ziwa.
“Aliniambia kuwa Masele ana
dili la shilingi milioni 180,
baada ya ujumbe huo
nilipokea simu ya waziri huyo
ambaye aliniambia
nikifanikisha nitalipwa fedha
hizo,” alisema.
Alisema kuwa Masele alimtaka
aeleze helikopta hiyo itatua
wapi, muda gani na kama
kweli wahusika wamo ndani
yake kisha ulipuaji ufanywe na
watu walioandaliwa.
Alisema alijiandaa na
kufuatilia ila hofu ya kimungu
ilimuingia akahofia taifa
litapokeaje tukio la kifo cha
Dk. Slaa na yeye akihusika.
“Nilimweleza Masele lakini
alimpigia simu mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Anna
Rose Nyamubi, ambaye
alimshauri kuwa sio vyema
tukio hilo likafanyika wilayani
kwake, baadaye
nilikutanishwa na katibu mkuu
wa umoja wa vijana ccm
(UVCCM) Taifa , Sixtus
Mapunda pamoja na mtu
mmoja wa usalama, ” alisema.
Aidha, alisema aliwashauri
badala ya kulipua watumie
mabango na kurubuni vijana
kuhujumu ziara ya Dk. Slaa
ambapo walifanikisha hilo.
Alisema baadaye walikutana
tena na Nape, Nchemba na
kuombwa wawashawishi
madiwani na viongozi
wengine wahamie CCM kwa
ahadi ya kupewa ukatibu wa
Wilaya kwenye wilaya
watakazoamua.
Alisema baadaye madiwani
hao walienda Mwanza mjini
ambapo huko walikutana na
Nape ambaye alieleza
kusikitishwa kitendo cha
Chadema kumvua
uwanachama Zitto.
KUONDOKA CHADEMA
Alisema Februari 26, mwaka
huu waliondoka rasmi
Chadema ambapo Nape alifika
huko na kukutana naye hoteli
ya Kalena ambapo katika
mazungumzo alimhakikishia
maisha mazuri pamoja na
uongozi.
“Usiku ulipofika gari la
mwenyekiti wa mkoa wa
Mwanza iliwachukua na
kuwapeleka uwanja wa ndege
na kusafiri kuja Dar es Salaam
kukutana na Nchemba ambaye
naye aliwataka waelekee
Dodoma na baadaye Kalenga,”
alisema.
Aliongeza kuwa Dodoma
walienda nyumbani kwa
Kinana ambaye huko
waliwakuta Masele, Nchemba
na Mchange ambapo wakati
wote Katibu Mkuu alisifu
kitendo chao cha kuondoka
Chadema.
Alisema katika mazungumzo
makada hao walimwambia
Nchange asichoke kwa kazi
anayofanya.
ACT YATAJWA
Mzuka alisema makada hao
walikubaliana mgogoro ndani
ya Chadema lazima uboreshwe
na kuahidi kugharamia fedha
za kwenda mikoani na pia
wakasema kuna chama
kitasajiliwa.
Pia alisema makada hao
walisema watahakikisha Msajili
wa vyama vya Siasa, Jaji
Francis Mutungi anakipatia
usajili wa kudumu kwa
gharama yoyote chama cha
ACT ili CCM ipate ushindi
kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema katika mazungumzo
hayo, Kinana alisema ACT
imeanzishwa kwa lengo
maalum la kuipa CCM ushindi
kwa kuwa hata huko duniani,
ushindi wa chama tawala
unatokana na usajili wa vyama
vipya.
WABUNGE WANNE
KUHUJUMIWA
Makada hao walikubaliana
katika uchaguzi ujao mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu
Lissu, asirudi bungeni kwa
sababu ameitia hasara serikali
kuhusu hoja zake dhidi ya
katiba.
“Katika jimbo la Lissu, ACT
itafadhiliwa kusaidia kutoa
mgombea CCM ambapo
itagawa kura za jimbo,”
alisema.
Diwani huyo alitaja wabunge
wengine ambao wapo kwenye
mtego huo kuwa ni mbunge
wa Arusha mjini, Godbless
Lema ambaye imeelezwa
amesababisha kushuka kwa
utalii.
Wengine ni mbunge wa Iringa
mjini Mchugaji Peter Msigwa
na mbunge wa Mbeya mjini,
Joseph Mbilinyi.
Kwa upande wa Lissu alisema
kwa mujibu wa sheria ya
uchaguzi wa serikali za mitaa,
Diwani akijiuzulu anatakiwa
aandike barua rasmi kwa
mwenyekiti wa Halmashauri
na kuambatanisha na kiapo.
“Hawa hawakufanya hivyo kwa
hiyo bado ni madiwani wa
halmashauri ya mji wa
Shinyanga,na uthibitisho kuwa
hawajajiuzulu ni kuwa siku 90
zimepita bila kutangazwa
uchaguzi, “ alisema.
NIPASHE

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top