Unknown Unknown Author
Title: UN YALAANI MATESO YA WAKRISTO IRAQ
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mapambano Iraq Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Jihad wa Iraq dhidi...


Mapambano Iraq
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Jihad wa Iraq dhidi ya wakristo wa eneo wanalolishikilia.
Hii ni baada ya kikao cha dharura cha baraza hilo ambalo lilikutana kujadili hali mbaya ya maeneo ya wakristo, baada ya wapigani wa Jihad kushikilia eneo walilokuwa wakilikalia.

Tayari Marekani inafikiria kuchukua hatua dhidi ya wapiganaji hao lakini makao makuu ya jeshi la nchi hiyo Pentagon limekana taarifa kuwa limeanza mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji hao.Baraza hilo limeomba jamii ya kimataifa kusaidia serikali ya Iraq. Maelfu ya wakristo na wengine wasio na uwezo wamekuwa wakiwakimbia wapiganaji wa Jihad kaskazini mwa Iraq.
Naye Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amewaomba viongozi wa dunia kusaidia kusitisha machafuko kaskazini mwa Iraq baada ya wapiganaji kutoka kundi la kiislam kuukamata mji wa Qaraqosh, mji wenye wakristo wengi katika ukanda huo. Maelfu ya wakristo wameyakimbia makazi yao kuelekea maeneo ya milimani. Msemaji wa Vatican, Frederico Lombardi amesoma tamko la Papa akiisihi jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua:
"Baba mtakatifu anatangaza ombi kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ili kumaliza ukatili unaoendelea, kuwalinda wale walioathirika au kutishiwa na vurugu na pia kuwapa misaada hasa mahitaji ya haraka kwa wengi ambao wamelazimishwa kuhama na wale walio tegemezi," Amesema Lombardi
Wakimbizi wa kikristo wanaokimbia eneo linaloshikiliwa na wapiganaji wa Jihad
Zuhair Al Nahar anayeishi London ni msemaji wa Al Dawaa chama cha waziri mkuu wa Iraq Nouri Al Maliki amesema hali ni tete na serikali huko Baghdad inahitaji msaada wa kimataiafa:
"Tunahitaji usaidizi. Tunahitaji jumuiya ya kimataifa kuingia na kuchukua jukumua la kupambana na hii laana ya magaidi. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuamka na kutambua kuwa huu ndio wakati wa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya hawa magaidi," Amesema Al Nahar
Ali Khedery alihudumia serikali ya marekani kwa muda mrefu katika Iraq anasema Marekani inahitajika kuchukua hatua ya kijeshi na pia kutoa msaada Zaidi kwa uongozi wa wakurdi.
"Msaada wa anga kwa kutumia ndege za kijeshi za marekani nadhani unahijika, na nadhani ni busara kuwaruhusu waliko katika kilele cha mlima cha Sijar kutoroka. Lakini unatakiwa kuzingatia kipi kitatokea baadae. Kitakachofuata baadae ni kuwa wataingia katika Kurdi na wataungana na waarabu wengine wasio na makazi katika Iraq wapatao milioni moja na nusu na Wasiria wengine walioingia kurdi hali itakayoongeza msongo kwa utawala wa wakurdi ulioko katika eneo hili," Amesema Khedery
BBC SWAHILI

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top