WHO YASAKA MIKAKATI KUPAMBANA NA EBOLA
Vita dhidi ya Ebola, homba ambayo ni janga kubwa Afrika Magharibi
Wataalamu wa maswala ya Afya ulimwenguni kutoka WHO wanakutana kujadili hatua mpya za kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Mkutano huu wa siku mbili unafanyika mjini Geneva , Switzerland na utaamua kama watatangaza hali ya hatari kiafya ulimwenguni ambayo itahusisha kuzuia safari katika maeneo yaliyoathiriwa na Ebola.
Ugonjwa huu ulijitokeza Mwezi Februari mwaka jana na tangu wakati huo ukasambaa kwenye nchi nne za Afrika, na kusababisha watu 900 kupoteza maisha.
Ugonjwa huu umekua hatari zaidi kiasi cha kufanya wataalam wa afya kutumia jitihada kubwa zaidi kupambana nao.
Wafanyakazi wawili kutoka Marekani walioathirika na ugonjwa wa Ebola nchini Liberia wameelezwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupatiwa dawa ambayo haijathibitishwa kwa matibabu kabla ya kurudishwa nchini Marekani.
Lakini haifahamiki kama dawa aina ya Zmapp ambayo ilifanyiwa majaribio kwa Nyani inaweza kuthibitishwa kuwa bora.
Profesa Peter Piot aliyegundua Ebola mwaka 1976,Profesa David Heymann mkuu wa kitengo cha usalama wa afya duniani na mkurugenzi wa mfuko wa Wellcome Profesa Jeremy Farrar wamesema kulikua na dawa aina kadhaa na chanjo walizogundua kwenye utafiti wao ambazo zinaweza kutumika dhidi ya Ebola.
Katika kauli yao ya pamoja wataalam hao wamesema nchi za kiafrika ziruhusiwe kuamua kutumia au kutotumia dawa hizi, kwa mfano kuzuia na kutibu wafanyakazi wa idara za afya ambao wako katika hatari ya kuambukizwa
BBC SWAHILI
Post a Comment