Pichani ni mwonekano wa mifereji ya kupitishia maji taka ya mvua ikiwa imezibwa na taka ngumu za wafanya biashara wa mji mdogo wa Mlowo
Kamera yetu leo asubuhi ili angazia kiapnde cha barabara ya lami cha Kamsamba eneo la Mji mdogo wa Mlowo,
Timu ya MJUMBE BLOG ime shuhudia uharibifu wa miundombinu ulio zoeleka kwa wakazi wa mitaa hiyo.
Uharibifu huo umetokana na utupaji hovyo wa taka ngumu unao fanywa na wafanyabiashara,wachuuzi,mafundi seremara,mafundi karakana wanao tumia mifereji ya kupitishia maji ya mvua katika barabara hiyo kama madampo yao.
Matokeo yake wame sababisha uharibifu mkubwa wa kipande hicho cha lami ambacho kime anza kumomonyolewa kwa kasi.
Mamlaka zinazo huska zina chelea haya kwa makusudi au kwa mazoea jambo ambalo miaka ya usoni lita igharimu serikali kwani ita takiwa kurudia au kuanza upya kuijenga bara bara hiyo kwa kodi za wananchi ambazo kama hatua za haraka zingechukuliwa mapema fedha hizo zinge tumiwa kufanyiwa kazi zingine kijamii au kuendelezea kipande cha lami zaidi kuelekea Kamsamba.
Rai yetu:Salaam ziwafikie wahusika waelewe jamii iliwapa dhamana ili iwatumikie kwa vitendo na sio kukaa maofisini kupiga porojo.
Maelezo na Picha Zote
Timu ya MJUMBE BLOG
Mbeya,Mlowo



Post a Comment