Unknown Unknown Author
Title: LUKUVI:NITAPAMBANA NA RUSHWA WIZARA YA ARIDHI!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LUKUVI AAHIDI KUPAMBANA NA RUSHWA WIZARA YA ARDHI Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewatak...

LUKUVI AAHIDI KUPAMBANA NA RUSHWA WIZARA
YA ARDHI
Waziri mpya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewataka
watendaji wa wizara hiyo wanaojihusisha na
vitendo vya rushwa kuachia ngazi mara moja,
vinginevyo watakiona cha moto.
Akizungumza kwa mara ya kwanza na
wakurugenzi,
maofisa na watendaji wakuu wa wizara hiyo
aliporipoti katika makao makuu ya Wizara hiyo
Lukuvi alisema "Ninawachukia sana wale wote
wanaojihusisha na vitendo vya kuwakumbatia watu
wenye pesa na kuwanyanyasa walalahoi wa nchi
hii
kwa kujali masilahi yao."
"Nimeingia hapa nikijua kabisa kwamba watu hao
wapo, na nikijua kuwa wizara hii ni kaa la
moto,lakini mie si mgeni najua kila kitu
kinachotendeka hapa. Baadhi ya watendaji
wizarani
wamegeuka miungu watu, wenye dhuluma,
waonevu, wasiotenda haki, watu wakujali wenye
pesa, kuanzia kwa wanyonge hadi wizarani,”
alisema Lukuvi.
"Nitahakikisha watu hao ninapambana nao na
kuhakikisha wanajali misingi ya utumishi wa
umma;
pia nitaenda hadi mikoani kuwasikiliza wananchi
ambao hawana hata senti tano nitawafuata huko
huko nikasikilize kero zao, kwani wananchi wengi
hawana nauli ya kufika Dar es Salaam," alisema.



Karibu Ututembelee MJUMBE BLOG mtandaoni kwa Picha za matukio mbalimbali,Matangazo,Habari na Taarifa mpya ya masuala mbali mbali ndani na nje ya nchi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top