Unknown Unknown Author
Title: MAJAMBAZI 40 YATEKA BASI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WATU zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa majambazi, wameteka mabasi sita ya abiria yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, ...

WATU zaidi ya 40 wanaodhaniwa kuwa
majambazi, wameteka mabasi sita ya abiria
yanayofanya safari zake kati ya Jiji la Arusha na
Nairobi, Kenya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema atalitolea ufafanuzi leo. Kamanda
alisema mabasi hayo yalitekwa juzi saa 8 usiku,
baada ya kufika eneo la Mbuga Nyeupe, Wilaya
Longido, Mkoa Arusha.
Taarifa zilizopatikana jijijni Arusha , zinasema
baada ya majambazi hayo kuteka mabasi hayo
yaliyokuwa yakitokea Nairobi kuelekea Arusha,
waliwapora mali na fedha abiria wote.
Taarifa hizo, zinasema majambazi hayo yaliweza
kufanya uhalifu huo baada ya kuweka mawe
barabarani, na baada ya kuyateka mabasi hayo,
waliwaamuru abiria wote kushuka na kulala
chini, huku wakipekuliwa na kuwataka
wasalimishe mali zote walizokuwa nazo.Dereva
wa moja ya mabasi yaliyotekwa, mali ya
kampuni ya Perfect Trans, Joseph John,
aliwaambia waandishi wa habari kuwa
majambazi hayo yalikuwa na silaha za jadi
yakiwemo mapanga na mashoka. "Kundi na
majambazi lilikuwa kubwa yaani walikuwa kama
watu arobaini hivi, wametufanyia unyama wa
kutisha kwa sababu wanawake walivuliwa nguo
na vito vya thamani na wanaume tukivuliwa
viatu na kuporwa kila kitu". Tukio hilo lilidumu
kwa muda wa dakika 20, kwani kila walipokuwa
wakimaliza kupekua abiria waliwamuru warudi
ndani ya basi na kuhamia basi jingine alisema
dereva huyo. Pamoja na hayo, alisema kuna haja
Jeshi la Polisi kurudisha ulinzi uliokuwa
ukifanywa na magari ya doria katika barabara ya
Arusha-Namanga uliondolewa Aprili, mwaka
jana.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top