Unknown Unknown Author
Title: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA WANANCHI(JWTZ)!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa wananchi na Vyombo vya Habari kuhusu mgogoro wa eneo la TONDORONI li...

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
linapenda kutoa taarifa kwa wananchi na
Vyombo vya Habari kuhusu mgogoro wa
eneo la TONDORONI lililopo katika Wilaya
ya Kisarawe kama ilivyokaririwa na baadhi
ya Vyombo vya Habari hapa nchini.
Taarifa zilizotolewa na kukaririwa na
baadhi ya Vyombo vya Habari kwamba
Wanajeshi wametumia nguvu kuwatoa
wananchi eneo la TONDORONI na baadhi
yao kudai kupotelewa na mali zao siyo za
kweli na ni za kuwapotosha wananchi
kwa sababu wananchi hao walitaarifiwa
kuondoka kupitia uongozi wa Wilaya na
uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na
KILUVYA B. Aidha, walipewa muda wa
kutoa vitu vyao na wao kuondoka.

JWTZ linapenda kuwahakikishia wananchi
kuwa hatua ya kuwaondoa wananchi
wavamizi kutoka katika eneo la kambi ya
Jeshi kwa uangalifu, umakini na kulikuwa
na usimamizi wa hali ya juu na hakuna
mali ya mwananchi iliyoporwa kama
ilivyodaiwa. Ifahamike kwamba; Jeshi
linaona ni bora lilaumiwe kwa kuwaondoa
wananchi waliovamia maeneo hatarishi ya
jeshi ambayo hutumika katika mafunzo
yanayohusisha risasi za moto, zana hatari
za kijeshi na mabomu ambayo wakati
mwingine hulipuka baada ya muda fulani
kupita badala ya kuwaacha wakae katika
maeneo hayo kutokana na sababu za
kisiasa au ushabiki mwingineo na hivyo
kuwa katika hatari ya kuweza kuumia
vibaya au kupoteza maisha yao na mali
zao.

Pia ni vema tukajua historia ya tatizo hili.
Mnamo mwaka 1978 eneo linalojumuisha
vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B na
kilichokuwa kijiji cha TONDORONI
lilichukuliwa na Serikali kwa ajili ya
matumizi ya JWTZ. Baada ya maamuzi
hayo Kikosi cha JWTZ kilihamia
TONDORONI mwaka 1981na kukalia eneo
la hekta 4197. Serikali ililipima eneo la
TONDORONI kisheria mwaka 1984 na
eneo lote liliwekewa mawe ya mipaka.


Tutembelee MJUMBE BLOG Mtandaoni kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na Matukio mbali mbali yanyao gonga vichwa vya habari kila mara.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top