Unknown Unknown Author
Title: THAMANI YA SHILINGI YETU ILI WAHI KUSHINDANA NA DOLA 1 YA MAREKANI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JE, UNAJUA SHILINGI YETU ILIWAHI KUSHINDANA NA DOLA? Mwaka 1961 wakati Tanzania inapata Uhuru chini Mwalimu Nyerere Dola 1 ya Marekani i...

JE, UNAJUA SHILINGI YETU ILIWAHI KUSHINDANA
NA DOLA?
Mwaka 1961 wakati Tanzania inapata Uhuru chini
Mwalimu Nyerere Dola 1 ya Marekani ilikuwa sawa
na Sh7.14 za Tanzania, hali hiyo iliendelea mpaka
mwaka 1972. Mwaka 1973 Dola 1 ilikuwa sawa na
Sh7.3 ya Tanzania. Mwaka 1984 Dola 1 ilikuwa
sawa na Sh15.29 na wakati Nyerere anakabidhi
madaraka kwa Ali Hassan Mwinyi mwaka 1985
Dola 1 ilikuwa sawa na Sh17.47. Miaka hii ndipo
nchi ilikuwa vitani, kuikomboa Uganda.
Miaka 10 ya Rais Mwinyi ilishuhudia shilingi
ikiporomoka kama utelezi, kutoka shilingi 17.47
kwa dola 1 mwaka 1985 mwishoni, hadi shilingi
574 kwa dola 1 mwaka 1995. Serikali ya Mwinyi
ilisifika kwa kukopa, wakati nchi inakabidhiwa kwa
Mkapa, tulikuwa tunadaiwa trilioni za shilingi.
Wakati Mkapa anaanza uongozi wa nchi, dola 1 ya
Marekani ilikuwa sawa na shilingi 574.76 za
Tanzania. Miaka 10 baadaye wakati anamaliza
muda wake (Dusemba 2005) Dola 1 ya Marekani
ilikuwa sawa na shilingi 1089.34 za Tanzania.
Utawala wa Mkapa ulikuwa na kibarua kigumu cha
kulipa madeni yaliyokopwa wakati wa Mwinyi.
Wakati Kikwete anakabidhiwa nchi mwaka 2005,
dola 1 ya Marekani ilikuwa sawa na Shilingi
1,128.93 za Tanzania, miaka 10 baadaye (yaani
mwaka huu 2015), Dola 1 ya Marekani ni sawa na
shilingi 1778.70,
Nina uhakika kuwa, wakati Kikwete atakuwa
anaondoka madarakani mwezi Desemba mwaka
huu, Dola 1 ya Marekani itakuwa sawa na zaidi ya
shilingi 2100 za Tanzania. Uongozi wa Kikwete
umesifika kwa kuendelea kukopa zaidi. Hivi sasa,
deni la taifa limeongezeka na kufikia takribani
trilioni 30 za kitanzania, na huwenda wakati
Kikwete anaondoka madarakani, deni la taifa
likawa takribani trilioni 31 au 32.
Mungu Ibariki Tanzania.
J. Mtatiro,
19 Jan 2015.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top