Unapo kuwa maeneo ya wilaya ya Mbozi,eneo maarufu kwa Kilimo cha zao la Mpunga utaambiwa Kamsamba!
Msimu wa mavuno unapo wadia pia.Shehena za Mpunga kwenye Malori na Stoo mbali mbali katika miji kama Mlowo na Vwawa hufurika kwa wingi.
Ambapo unaweza kwenda Kukoboa Mpunga lakini Uka ambiwa wiki hili ni Zamu ya flani tu kukoboa mpunga,Kama una hitaji huduma basi weka foleni...
Lakini ukitembea Masoko yote ya Miji ya mbali mbali ndani ya Mbeya kamwe hauwezi kuona bandiko linalo Onesha kuuza MCHELE WA KAMSAMBA.
Najiuliza kunani?
Imani yangu ni kuwa Mchele wa Kamsamba Upo masokoni,Lakini inakuwaje hautangazwi?
Hapa nina uona ule Mchezo wa wafanya buashara uitwao MAGAZIJUTO!
Mchezo wa kucheza na akili za wateja wao.
Isije ikawa;
MCHELE ule wa Kamsamba ndio unaitwa MCHELE SUPER WA KYELA!! Maana kwa macho na utashi wangu mimi huwa nina Amini kuwa MCHELE ni Mmoja! Ila Majina ndio tofauti.
Kwahiyo ipo hivi;Mchele wa Kamsamba unaitwa jina hilo mpaka ukivuka Mto Momba...
Ukisha vuka getini Igamba na kushushwa pale chamani Unabatizwa jina la MCHELE SUPER WA KYELA Unapatikana hapa!!
Nasema Isije Ikawa!!
Mi simo.
Ndimi Mdau wa MJUMBE BLOG niitwae 'MCHAGUA JEMBE'.
MJUMBE BLOG
Tunakushukuru kwa kututembekea.
Kwa matangazo na Maoni piga 0752025002.
Post a Comment