Picha ya kwanza hapo chini Mwl. Marry Masombuka ( Jina
halisi Whoopi Goldberg) akitiwa nguvuni na vikosi
vya Makaburu kwa kuwafundisha wanafunzi
historia ya kweli badala ya ile ya uwongo
iliyolenga kuwatukuza wakoloni.
Picha ya pili hapo juu ilichorwa kuonesha vikosi vya
Napoleon vikiukimbia mji wa Moscow ukiwaka
moto.
Kwa wale ambao.
Na:Ado Shaibu
FILAMU YA SARAFINA NA KUCHOMWA KWA JIJI
LA MOSCOW
Hivi karibuni nimerudia tena kuitazama filamu ya
Sarafina, filamu ambayo wengi wetu ilitukonga
sana nyoyo enzi zile tukiwa makinda. Wakati huo,
pamoja na mambo mengine, wengi tulikunwa hasa
na nyimbo zilizosheni kwenye filamu na harakati
za wanafunzi wa Soweto dhidi ya serikali ya
Kikaburu. Lakini, wakati huo, umri na uelewa wetu
mdogo vilitunyima kuyaelewa kwa kina yaliyokuwa
yanazungumzwa kwenye filamu.
Awamu hii, uelewa wangu wa filamu hii
umepanuka kiasi baada ya kukisoma kitabu cha
“Glimpses of World History” chenye mkusanyiko wa
barua ambazo mwanasiasa mashuhuri wa India
Jawaharlal Nehru alimwandikia Bintiye Indra
Gandhi wakati ambao Nehru alikuwa gerezani
kutokana na kushiriki kwake kwenye harakati za
kupigania uhuru wa India.
Kwenye kitabu cha Nehru, zipo barua mbili kuhusu
Napoleone Bonapatre, yule mtawala mbabe wa
Ufaransa aliyewanyima usingizi watawala wenzake
wa Ulaya kwa mfululizo wa vita zake almaarufu
kama “Vita za Napoleon”.
Katika barua hizo ( Barua ya 404 iitwayo
“Napoleon” na barua ya 405 iitwayo “More About
Napoleon”), Nehru anamjuza mwanaye, pamoja na
mambo mengine, kuhusu kisa cha kuchomwa moto
kwa jiji la Moscow mwaka 1812.
Mwaka huo, Napoleon aliivamia Urusi. Vikosi vya
Napoleon, “La Grand Armee” kama vilivyoitwa kwa
umadhubuti wake, vilisonga mbele bila upinzani
mkubwa. Mwishowe, Napoleon akaliteka jiji la
Moscow.
"Ili kumwondosha Napoleon, Warusi
walichukua uamuzi mgumu. Ofisi muhimu na
majengo vilichomwa moto. Strange as it may
seem, moto huo ulimwondosha Napoleon Moscow."
Upo mjadala na versions nyingi kuhusu kuchomwa
kwa jiji la Moscow, mjadala ambao nisingependa
kuuendea kwa kina leo.
Tukirudi kwenye filamu yetu ya Sarafina, kati ya
maeneo ninayoyahusudu zaidi ni pale Mwalimu
Mary Masombuka ‘akishusha nondo’ za historia
kwa wanafunzi wake.
Kwa Mary Masombuka,
historia ni nzuri na hutufanya tujifunze fahari yetu
japo wakati mwingine yaweza kukufanya utokwe na
machozi.
Chambilecho yeye mwenyewe, “History is
so beautiful..it makes you cry…’’
Kwa mlioitazama filamu, mtakumbuka kipande
ambacho Masombuka alikuwa akifundisha kuhusu
kushindwa kwa vikosi vya Napoleon. Kwamba
watu wenyewe waliamua kuutia moto mji wao ili
kumfukuza adui. Kwa lugha nyepesi, umma
ukiamua, unaweza kuchukua hatua inayoweza
kuduwaza kama hii ya kuutia mji kiberiti ili tu
kumshinda adui. Na kwa hakika, hakuna aliyewahi
kuishinda nguvu ya umma. Tujikumbushe maneno
ya Masombuka mwenyewe:
So what do we learn from this?
Napoleon Army…
The best equipped…
The best trained army..
The most powerful army on the continent
….So what happened? They were defeated by the
people. PEOPLE CAN DEFEAT THE ARMIES. History
has proved that!
Credit:Kitabu Nilicho Kisoma.
MJUMBE BLOG
Tuna shukuru kwa kututembelea na kutumia Huduma zetu.
Hahshs ..... Jsjsjs

Post a Comment