Aliyekuwa MNEC wa wilaya ya Ludewa
Elizabeth Haule wa pili kushoto enzi za
uhai wake akiwa na viongozi wa wilaya
hiyo wakati wa mkutano mkuu wa wilaya
ya Ludewa mwaka jana ,kulia ni mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe ,aliyesimama ni mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley
Kolimba na wa kwanza kushoto katibu wa
CCM wilaya ya Ludewa Eliud Semauye.
CHAMA cha mapinduzi (CCM) wilaya ya
Ludewa mkoani Njombe kimepata pigo
kubwa kufuatia kifo cha aliyekuwa mjumbe
wa Halmashauri kuu ya wilaya hiyo (NEC)
Bi Elizabeth Haule.
Mbali ya kuwa MNEC wa wilaya hiyo
Haule pia alikuwa ni mwenyekiti wa
UVCCM wilaya ya Ludewa kabla ya
kujiuzulu kwake mwezi February mwaka
jana baada ya kuchaguliwa nafasi hiyo ya
NEC na nafasi hiyo kuwa wazi hadi sasa.
katibu mwenezi wa CCM wilaya ya
Ludewa Felix Haule alisema kuwa kifo cha
kionozi huyo kimetokea usiku wa kuamkia
leo akiwa katika Hospitali ya wilaya ya
Ludewa ambako alilazwa jana mchana
kwa tatizo la moyo.
Bw Haule alisema kuwa siku ya jumatatu
wiki iliyopita marehemu alipata kuongoza
kikao chake cha mwisho cha baraza la
vijana la wilaya ya Ludewa na baada ya
hapo hali yake ya afya ilianza kuzidi kuwa
mbaya zaidi kabla ya kuamua jana
kwenda Hospitali ambako walimlaza
Alisema kuwa mazishi ya mjumbe huyo
wa NEC wilaya ya Ludewa yanataraji
kufanyika kesho kutwa jumamosi kijijini
kwake Mholo kata ya Luana wilayani
Ludewa .
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la
Ludewa Deo Filikunjombe akielezea kifo
cha MNEC huyo alisema kuwa amepokea
kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo
hicho na kuwa kwa sasa anafanya
maandalizi ya kuelekea jimboni Ludewa ili
kuungana na wana CCM na wananchi wa
wilaya hiyo katika mazishi ya kiongozi
huyo.
MJUMBE BLOG Tuna shukuru kwa Kututembelea!
KARIBU TENA
Post a Comment