Unknown Unknown Author
Title: UJUMBE KWA WAHUDUMU:"HATUHITAJI KUSIKILIZA SAUTI ZENU NYORORO;TUNA HITAJI HUDUMA"
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Assumpta Nalitolela Nimeandika makala kadhaa zinazohusu huduma bora kwa wateja katika safu hii. Nalazimika kuandika tena leo kwa sab...

Na Assumpta Nalitolela

Nimeandika makala kadhaa zinazohusu huduma
bora kwa wateja katika safu hii. Nalazimika
kuandika tena leo kwa sababu kwa kweli maeneo
mengi ya nchi hii huduma ni mbovu sana. Yapo
mabadiliko katika maeneo machache ambayo
yanaonyesha angalau watu wanatambua kuwa
kuna ushindani katika biashara zetu hivyo
wanatakiwa kutoa huduma kwa ushindani; hao
nawapa hongera.

Watu wengi bado wanababaika ni namna ya
kuhudumia kwa ushindani. Wapo wale ambao
wanaamini kwamba kutabasamu, kusema karibu
na nikusaidie nini ndio mambo ya msingi ya
kumfanya mteja abaki kwenye biashara yako.

Ni kweli mambo hayo ni ya msingi lakini kama
mteja hatatatuliwa tatizo lake lililomleta kwa
mtoa huduma mambo hayo ya kutabasamu
yanakuwa hayana maana. Ni bahati mbaya
kwamba tabia za watoa huduma wetu wengi
zinaonesha kuwa na fikra hii; na hii ni hatari
kwa ustawi wa biashara.

Tembelea maeneo
mengi ya huduma hata zile za taasisi kubwa
utayakuta hayo. mifano ifuatayo ni kielelezo cha
malalamiko yangu.
Unakwenda kwenye taasisi kutaka kujua kitu
fulani halafu unakutana na mtoa huduma
ambaye ameandaliwa kujibu maswali yako lakini
hana hata habari kwamba hicho unachotaka
kukijua kipo kwenye taasisi yake.

Nakumbuka nilishawahi kwenda kwenye duka
kubwa tuu nikitafuta moja ya vifaa
vinavyoturahisishia shughuli zetu za jikoni.
Nilikaribishwa vizuri sana na binti aliyekuwa
katika duka hilo huku akionesha uso wenye
tabasamu na ukarimu.

Hilo likaisha na mimi ninayejali sana huduma
ninayopewa na wengine nikaridhika kwa hatua
hiyo ya awali ya utoaji wa huduma.
Hata hivyo, nilipofika hatua ya pili sasa ya
kupata ufumbuzi wa hicho kifaa cha jikoni
nikakwama. Chombo kile kilikuwa tofauti na vile
nilivyovizoea; kulikuwa na vifaa vya ziada
ambavyo sikujua nitavitumiaje.

Nikaomba msaada kwa mhudumu wangu
aliyenikaribisha vizuri sana lakini cha kusikitisha
alikuwa hata hajui hicho kifaa ni cha nini.
Kwa kweli yale yote aliyoyafanya awali
yakayeyuka katika kichwa changu kilichobakia ni
maswali mengi ambayo mengine nilimuuliza
hapohapo kwamba inakuwaje mtu anauza kitu
asichokijua hata ni kitu gani.

Kwa kweli
nilikasirika. Nikashindwa kununua kifaa kile na
kuondoka.
Jamani watanzania wenzangu ndio nini hii.
Unajiitaje mtoa huduma kama hujui hata kama
hicho unachokiuza? Kwa ufahamu wangu ni
kwamba mtu muuzaji anapaswa kujua jina la
bidhaa yake, inatumikaje, mambo kadha wa
kadha yanayoambatana na bidhaa ile, bei yake.
Unakwenda dukani eti mhudumu hajui bei ya
bidhaa mpaka hapo atakapofika mtu anayejua;
kwa nini mtu huyo auze bidhaa hiyo.

Aina nyingine ya wahudumu wanaonikera sana ni
wale wanaotoa ahadi ambazo hawana hata
uhakika kama watakuwa na uwezo wa
kutekeleza.

Mfano hai nilionao katika kampuni moja ya simu
ambayo nilipewa ahadi, hili ni ahadi ambayo
nimekuwa nikipewa na watoa huduma wa
kampuni ya simu(Jina limeondolewa kama kulistili).
kwa kipindi cha zaidi ya mwezi
moja lakini mpaka leo hii sijapata suluhisho.
Nilituma shilingi 20,000 kwenye kampuni hiyo
nikitaka kuuziwa umeme, mpaka leo hii sijapata
umeme na wala sijarudishiwa fedha.
Hiyo ilikuwa 11/1/2015. Nilishapata taarifa
kwamba siku hiyo kulikuwa na matatizo katika
mitambo ya Tanesco. Baada ya hapo nimekuwa
nikipiga simu (jina la Kampuni la simu) na kupokelewa na wahudumu
ambao wanakukaribisha kwa sauti nzuri na
baada ya kujieleza tatizo langu, wote wanasema

“mama leo kuwa tu na amani utapata tuu
umeme wako”.

Najua kabisa kwamba mimi ninapowapigia simu
nao wanaulizia Tanesco ambako ndiko
walikopeleka hela yangu ili nipate umeme, hivyo
ufumbuzi wa suala hili upo mikononi mwa
Tanesco. Nawapelekea wao malalamishi yangu
kwa sababu fedha yangu ilipitia kwao.

Siwashangai wahudumu hao kwa kushindwa
kunipa umeme la hasha, ninawashangaa kwa
kutoa ahadi ya kutekeleza kitu kwa siku hiyo
hiyo wakati wanajua fika kwamba lazima
wawasiliane na taasisi nyingine.

Hawa ni wahudumu ambao wanafikiria
watamfurahisha mteja kwa kumwambia kuwa na
amani. Kweli maneno hayo ni mazuri kuyasikia
kwenye masikio ya mteja kama mimi lakini
hayafanyi mimi kupata umeme au kurudishiwa
fedha yangu. Ufumbuzi kwangu ni ama kupewa
umeme au kurudishiwa fedha. Kwa hiyo
tabasamu, maneno mazuri na ahadi hewa
havinisaidii mimi katika kupata umeme na fedha.
Watoa huduma wa nchi hii watambue kwamba
pale tunaposisitiza mtoa huduma kuwa na
tabasam lenye mvuto, lugha nzuri, mavazi safi
hatumaanishi kwamba hivi ndivyo vinavyotoa
suluhisho kwa matatizo ya mteja hapana.

Ni lazima njia sahihi zitumike ili kupata ufumbuzi
wa tatizo la mteja hapo ndipo tutakaposema
umemtendea haki mteja wako.
MWANANCHI.




MJUMBE BLOG
Tunakupa Pongezi za dhati kwa kuweza kututembelea.
HONGERA.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top