Unknown Unknown Author
Title: CHECK HII YA KOREA KASKAZINI;YAZINDUA SILAHA HATARI....
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Korea Kaskazini yazindua Silaha kali Serikali ya Korea Kusini inasema inaamini kuwa Korea Kaskazini inaweza kumiliki nyambizi kadha za kufan...


Korea Kaskazini yazindua Silaha kali

Serikali ya Korea Kusini inasema inaamini kuwa Korea Kaskazini inaweza kumiliki nyambizi kadha za kufanya mashambulizi kutoka baharini ndani ya miaka mitano inayokuja.

Hii ni baada ya Korea Kaskazini kuchapisha picha zilizomuonyesha kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un akitazama majaribio ya kuizindua nyambizi hiyo.

Korea Kusini imezikagua picha hizo za uzinduzi kwenye vyombo vya habari vya Korea Kaskazini na kusema kuwa ni za kweli.

Korea Kusini ilisema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa sana.

Sasa Korea Kusini na Marekani zinafikiria kuweka ngao ya mitambo ya kuzuia makombora kutoka Kaskazini hatua itakayogharimu mabilioni ya pesa.Korea Kusini ilisema kuwa uzinduzi huo ni suala linalochukuliwa kwa umakini na tahadhari kubwa

Hata hivyo haijulikani ikiwa makombora yanayofyatuliwa na nyambizi hiyo yana uwezo wa kubeba silaha za nuklia

Wadadisi wanasema kuwa Korea Kuskazini inaonekana kufanya mambo kwa kasi zaidi kuliko ilivyokisiwa kuunda zana zilizo na uwezo wa kushambulia kwa haraka.BBC SWAHILI

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top