Title: AFYA:MAKALA MAALUM KWA AJILI YA WANANDOA TU;TATIZO LA NGUVU ZA KIUME!
Author: Unknown
Rating 5 of 5
Des:
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi k...
Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha mwisho cha furaha katika maisha ya ndoa, kama
inavyofahamika, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa.
Hata hivyo, ili furaha ipatikane ni lazima tendo lenyewe lifanyike
katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili. Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’.
Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za
kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi
mwingine. Inaweza kuwa ni kujumuisha hali ya kutokuwa na uwezo wa
kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa
muda mzuri wa kutosha.
Licha ya hivyo, elimu mhimu kabisa ambayo mwanaume anapaswa kuifahamu
ni kuwa, nguvu hizi hazitoki katika madawa ya kemikali au pahala
pengine; zinatoka katika vyakula tu.
Tatizo la Nguvu za Kiume na Suluhisho lake
Kwanini wanaume huishiwa nguvu za kiume?
Kuishiwa nguvu za kiume ni jambo la kawaida kwa wanaume wengi. Ni
kushindwa kwa uume kudumu kusimama barabara kwa ajili ya tendo la ndoa,
au kuwahi kufika kileleni.
Hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume huongezeka kutokana na umri.
Kulingana na tafiti za kitabibu, wanaume wenye umri kuanzia miaka 60
tatizo hili ni kubwa kwao kuliko wanaume wenye umri wa miaka 40.
Wanaume wenye elimu ndogo juu ya utendaji kazi wa mwili na afya ndio
wanaokabiliwa sana na tatizo hili. Hii ni kwa sababu wanashindwa kuelewa
aina ya chakula kinachoongeza nguvu za kiume na za mwili kwa ujumla,
mtindo wa maisha wanayotakiwa kuishi ili kupunguza hatari hiyo,
wanakunywa pombe na hawafanyi mazoezi ya viungo. Mazoezi ya mwili hupunguza hatari ya kupungukiwa nguvu za kiume. Soma zaidi kuhusu mazoezi hapa => Hizi ndizo faida 50 za Mazoezi.
Tatizo la kupungukiwa nguvu za kiume linaweza kuwa na sababu za
kihisia (emotional causes) lakini sababu nyingine hutokana na maradhi
kama vile kisukari na shinikizo la juu la damu.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 hadi 60 ya wanaume wenye maradhi ya
kisukari wana tatizo la uume kushindwa kusimama. Watu wanaosumbuliwa na
kiharusi na ulevi nao wana hatari kubwa sana kwa sababu ya uharibifu wa
korodani (testicles) kutokana na ulevi sugu na kupoteza testerone. Pombe
hupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa manii (mbegu za kiume).
Watu wanaosumbuliwa na shinikizo la damu,
magonjwa ya tezi, majeraha (kama vile kutokana na upasuaji wa viungo
vya uzazi), matumizi ya dawa zenye kemikali bila mpangilio au ushauri wa
wataalamu na maradhi ambayo hudhoofisha mtiririko wa damu kwenye uume.
Hata hivyo, upungufu wa nguvu za kiume unatibika katika umri wa rika
zote.
Vipengele ambavyo daktari atahitaji kuvifahamu kabla ya kuanza kukutibu tatizo la kuishiwa nguzu za kiume ni;
Umri wa mgonjwa
Jumla ya afya aliyonayo kwa kwa sasa
Utendaji wa tendo la ndoa zamani na sasa
Migogoro ya ndoa, kifamilia, kazi n.k
Ni nini malengo ya tiba ?
Kuwa na mtaalamu mzuri ni njia ya kwanza katika kupata uponyaji
sahihi. Ni mhimu wewe kujisikia vizuri na kumwamini daktari wako,
kisaikolojia utakuwa umepiga hatua ya kwanza ya kupata nafuu ya tatizo
linalokukabili.
Nini Sababu ya uume kushindwa kusimama?
Kushindwa kwa uume kusimama pia hutambulika kama kuishiwa nguvu za
kiume. Ni kitendo cha mtu kushindwa kusimamisha uume au kudumisha
usimamaji wa uume kwa muda wa kutosha kufanya tendo la tendo na
mwenzake. Lakini wakati hii inaweza kumfikisha mwanaume katika upeo wa
raha (orgasm), hali hii yaweza kumuacha mwanamke akiwa hakutosheka.
Mke wako hupendelea ukawie ikibidi ukawie zaidi. Kama mwanaume atakuwa anawahi kumaliza, basi anakuwa hampi raha mke wake.
Ingawa, kama una tatizo la kuwahi kufika kileleni hauko peke yako.
Takribani asilimia 30 hadi 40 ya wanaume wa rika zote wana tatizo hili.
Lakini vile vile kufahamu tu kuwa wanaume wengine pia wana tatizo kama
lako haitakusaidia kuondoa shida inayokukabili.
Habari nzuri kwa wanaume ikiwa ni pamoja na wewe ni kwamba kuna njia zenye manufaa makubwa kabisa ya kumaliza tatizo hili.
Kuna wakati kushindwa kusimama uume kunaweza kuonekana kama si tatizo
lakini wakati hali hiyo inapoendelea kwa muda mrefu inaweza kuleta
hisia ya dhiki kubwa kwa mme na mke wake. Lakini hata hivyo, sababu za
kawaida zinazosababisha uume kushindwa kusimama ni pamoja na matatizo ya
mhemko kama;
Wasiwasi
Hofu
Msongo/Stress
Hasira
Huzuni
Ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa
Ili kuwa na uwezo wa uume kusimama panahitajika;
Mfumo wa neva ulio na afya nzuri ambao unapeleka mpwito neva (nerve impulses) katika ubongo, uti wa mgongo na uume.
Mishipa ya ateri iliyo na afya ya ndani na iliyo karibu na corpora cavernosa
Misuli laini yenye afya na tishu za ufumwele (fibrous tissues) ndani ya corpora cavernosa na
Kiwango sahihi cha oksidi nitriki (nitric oxide) ndani ya uume.
Kushindwa kwa uume kusimama kunaweza kutokea pia kama kipengele
kimojawapo katika hivyo vilivyotajwa hapo juu hakipo sawa. Pia sababu
zingine za kupunguwa kwa nguvu za kiume, kushindwa kwa uume kusimama, au
kuwahi kufika kileleni ni pamoja na;
Umri mkubwa zaidi
Kisukari
Kujichua/Punyeto
Uzinzi
Kukosa Elimu ya vyakula
Kutokujishughulisha na mazoezi
Shinikizo la juu la damu
Maradhi ya moyo
Uvutaji sigara/tumbaku
Utumiaji uliozidi wa kafeina
Kudhurika kwa neva au uti wa mgongo
Madawa ya kulevya kama vile bangi, heroini, kokeini, na pombe
Kiwango kidogo cha homoni ya testerone
Athari kutoka kwa baadhi ya dawa
Nguvu za kiume na mzunguko wa damu:
Nini kinachofanya uume usimame? Kwa haraka unaweza kusema ni msisimko. Ndiyo, unaweza kuwa sahihi. Lakini msisimko ni matokeo. Kuna kinachosababisha kutokea kwa msisimko huo. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anapaswa kuwa na jibu la swali hili ili atakapoona
tatizo ajuwe wapi pa kuanzia na pa kumalizia. Hata kama si kwa undani,
Elimu ya kujijuwa jinsi mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu
sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama wanavyodhani watu
wengi.
Kutokuwa na chochote kichwani kuhusu miili yetu inavyofanya kazi
ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia madawa kiholela na hivyo
kujidhuru badala ya kujitibu.
Kinachofanya uume usimame ni mzunguko wa damu. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji.
Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini na kama bado unasubiri kiu
ndipo unywe maji na tena unakunywa maji ya baridi! Nakupa POLE SANA
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na
hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na
kusimama kwa uume wako.
Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].
Kwanini mzunguko wa damu ni mhimu?
Mzunguko wa damu ulio katika afya bora husambaza damu ya kutosha
katika viungo vyote vya mwili hii ikijumuisha pia damu ya kwenye mishipa
ya uume wako. Hii ni kuwa hata kama utagusana na mwanamke hautaweza
kufanya chochote kama damu haizunguki katika viungo vyako kama
inavyotakiwa. Hebu mwangalie mtu aliyekufa, damu yake haizunguki, je
anafanya chochote? Hata hivyo huo ni mfano mkubwa sana.
Hii ni kusema kuwa, chochote ambacho kinazuia mtiririko wa damu
kwenda kwenye uume kinaweza kuzuia kusimama kwa uume. Kama mishipa ya
vena na ateri imeziba, mwili wako hautaweza kusimamisha uume vizuri. Hii
ni kutokana na kwamba uume hautapata damu ya kutosha.
Mara nyingi vena zilizoziba kutokana na mzunguko dhaifu wa damu ni
sababu ya kushindwa kusimama uume kwa wanaume wengi wenye miaka 60
kwenda juu, wanaume wenye kisukari na pia wanaume wenye hali ya kukauka
kwa vijiateri vya ateri, na wenye maradhi ya moyo.
Baadhi ya wanaume wanapatwa na tatizo la kuishiwa nguvu za kiume kama
matokeo ya kula vyakula vyenye mafuta mengi ambayo yanaweza kuzuia
mtiririko mzuri wa damu kwenye uume. Inashauriwa pia kuepuka vinywaji na
vyakula ambavyo husindikwa viwandani.
Katika tendo la ndoa kwa mwanaume, mishipa ya damu ya ateri ina
nafasi kubwa sana sababu ya kazi yake ya usafirishaji wa damu kwenda
sehemu mbalimbali za mwili, hivyo unashauriwa kujifunza namna ya kutunza
ateri za mwili wako ili kuruhusu mtiririko mzuri wa damu mwilini mwako.
Pia ni mhimu sana kuwaona wataalamu wa tiba kuhusu unavyojisikia na
jinsi unavyohisi kuwa pengine unaweza kuwa na tatizo katika mishipa yako
ya ateri. Jaribu kujiwekea utaratibu wa kujichunguza afya yako mara kwa
mara kama utahisi kunyemelewa na tatizo hili. Baadhi ya watu hufanya
maradhi kuwa sugu kwa sababu ya kuacha kujichunguza mara kwa mara hadi
wauguwe, huku ni kukosa kuelewa na kushindwa kujithamini na kujipenda
mwenyewe.
Jitibu tatizo la kupungua nguvu za kiume
Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko/stress
uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote.
Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi
kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi,
shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na
kuomba huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!. Soma zaidi kuhusu
mfadhaiko/stress hapa => [Dalili na Ishara 50 za Mfadhaiko/Stress.]
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi
ni vema ukajitibu kwanza na maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu
wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli,
kisukari, shinikizo la damu na hata uzito
ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na
kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma
kadhaa.
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni
kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize
mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali
vilevi kuliko hata afya yake hafai. Na kanuni ni hii; ukitaka uzuri ni
lazima udhurike kwanza. Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi
kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni
mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo
utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata
hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika
tatizo lako itakapojitokeza.
Vyakula vinavyotibu tatizo la nguvu za kiume ni pamoja na vifuatavyo:
Tangazo: Book Your Hotel Here:
1. Kitunguu swaumu
Kitunguu Swaumu
Chukuwa punje 8 mpaka 10 hivi za kitunguu swaumu, menya na uzikate
vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa
mwezi mmoja. Soma hii => [Kitunguu Swaumu Hutibu Magonjwa 30].
2. Tikiti maji
TikitiMaji
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote. Soma hii => [Faida 13 za Tikiti Maji Kiafya].
3. Ugali wa dona
Ugali wa Dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula
ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili
ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi,
chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali
wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote
tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia
yako kwa maisha yako yote.
4. Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita
kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia
chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku. Soma hii => [Ukweli kuhusu Chumvi na Maajabu yake].
5. Maji ya kunywa
Maji ni Uhai
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu
anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika
kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini. Soma hii => [Jitibu kwa kutumia maji mp3].
6. Mbegu za maboga
Mbegu za Maboga
Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila
kuziunguza. Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu
hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama
unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni
mhimu sana kwako.
7. Asali na Mdalasini
Asali & Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa,
ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja.
Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya
hivi kwa mwezi mmoja. Soma hii => [Asali na Mdalasini].
The part time Blogger love to blog on various categories like Web Development, SEO Guide, Tips and Tricks, Android Stuff, etc including Linux Hacking Tricks and tips. A Blogger Template Designer; designed many popular themes.
Post a Comment