Akizungumzia sula la Elimu,Mgombea ubunge alikaririwa akiwa ahidi wananchi wa kijiji cha Igamba kuwa kama watampa ridhaa akawa mwakilishi wao wa Jimbo la Mbozi atahakikisha anaunda mfuko wa Elimu wa jimbo ambapo alisisitiza kuwa hata kuwa tayari kusikia kuwa mtoto yatima/Masikini anakosa au ananyanyasika kupata Elimu ambayo ni haki yake ya Msingi,atahakikisha gharama za elimu yao zina lipwa na mfuko wa jimbo.
Pia katika elimu aligusia suala la kuhakikisha ata ishawishi serikari kujenga chuo cha veta ili wale wahitimu wanao kosa nafasi za kuendelea na masomo ya juu wajiunge katika chuo hicho kwa ajili ya kupewa elimu kwa vitendo kama nyenzo ya kukabiliana na changamoto/ulimwengu ulio mbele yao.
Katika sekta ya Afya alikaririwa akisema;
...sitakuwa tayari kusikia mama zangu wakidaiwa nyembe,madishi wala gharama za kiusumbufu wakati wa kujifungua...
...ni aibu sana akina mama wanao elekea kujifungua kuulizwa kama wana madishi au wembe badala ya kuulizwa jina na kuanza kupewa matibabu,kama mta nipa ridhaa nita hakikisha hilo lina kuwa historia katika hospitali/vituo vya afya katika jimbo langu la mbozi.
Akizungumzia kwenye suala la kilimo kwenye zao la kahawa katika jimbo la Mbozi ali gusia suala la kuhakikisha anashiriakiana na watafiti wa masuala ya kilimo cha kahawa na kuhakikisha nakuja na suluhu ya tatizo la kukosa mazao mengi,kupata miche bora zaidi ambayo baada ya miezi 18 inaanza kutoa matunda mengi pia,
...nita fanya mipango ya kupata miche bora na inayo toa matunda kwa miezi 18 tu ili imunufaishe mkulima;alisema Pascal Haonga.
kwenye kilimo aligusia suala la kodi kubwa ya ushuru wanayo tozwa wakulima,hapa aligusia kuwa kawaida ilitakiwa kutozwa kodi kati ya asilimia mbili na tano.Hili linge tegemeana na bei ya zoa la kahawa katika soko la dunia.Lakini kinacho sikitisha zaidi ni pale ambapo kila mwaka wakulima hukatwa asilimia tano bila kujali soko la kahawa lime kuwa zuri au baya jambo lililoifanya kahawa izidi kuwa nufaisha wengine na sio mkulima.
Suala la mahindi alisema 'kuhusu suala la zao lamahindi katika wilaya ya Mbozi hilo sita lizungumzia kwani kila mkulima na mwana nchi anajua alicho tufanyia huyu naibu waziri wa kilimo!
Sitaki nitoneshe majeraha zaidi...'
Nime kuwekea picha za matukio mbali mbali eneo kutoka eneo la tukio,kijijini Igamba,Mbozi kama zilivyo letwa hapa na mdau wetu.
Akiteta jambo na moja ya wagombea udiwani kata ya halungu
Mgombea Udiwani kata ya Igamba ndugu Zalbabel Nzowa alipo kuwa akipanda jukwaani kwa ajili ya kuongea na wana Igamba.
Pichani ni ndugu Tendam Mdolo,mgombea udiwani kata ya Itumpi kwa tiketi ya UKAWA/CHADEMA akiwapa salaaam wana Igamba.
Pichani ni Bi Ester Kayombo Mgombea udiwani viyti maalum kata ya akiwapa neno wana Igamba,
Sophia Mwabenga "Mama wa mahindi" akiwa funulia wana Igamba kuhusu fedha yao ya rudhuku aliyo ipigania kama mwana Igamba na misukosuko aliyo ipata katika kupigania fedha husika.
Pichani ni Ndugu Gwamakha Mbughi,Mjumbe wa kati kuu Taifa na moja ya Viongozi waandamizi CHADEMA mkoa.
....alipo ifananisha nchi yetu Tanzania na mtu mwenye Ng,ombe watano wa maziwa wa kisasananaye mwomba msaada ya mwenzake mwenye ng'ombe wawili!
Alizungumzia mfono huo alipo zitazama raslimali nchini Tanzania na maisha ya watu wake na mtindo wa Seerikari kutembeza bakuli kwa nchi wahisani kwa ajili ya bajeti kila mwaka.
Naam;Kazi na Dawa:
PICHA ZAIDI PASCAL HAONGA AKIBURUDIKA NA WAKAZI WA IGAMBA WALIO JITOKEZA KUMPOKEA NA KUMSIKILIZA;
















Post a Comment