
Polisi mkoani Njombe ktk mji mdogo wa Makambako wanashikilia gari moja aina ya Toyota Noah kwa kuhusika ktk tukio la wizi wa ng'ombe. Kilichovuta hisia za watu ni mbinu waliyotumia wezi hao kumsafirisha ng'ombe huyo kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah. Askari waliokuwa doria walishuku gari hiyo na kuisimamisha, lakini dereva hakusimama na akaongeza mwendo. Ndipo Askari waliifukuza na hatimaye dereva akasimama na kushuka yeye na watu wengine watatu na kutokomea porini wakitelekeza gari hiyo na ng'ombe ndani.
Post a Comment