Vijana wazalendo wa Taifa wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Vijana wazalendo wa Taifa wakionyesha uzalendo kwa kuonyesha skafu zao zenye jina la Tanzania

Ujumbe maalum na maridhawa katika msingi wa Muungano ulioasisiwa na waasisi wa Taifa letu ambao ni tunu ya umoja na mshikamano katika taifa letu endelevu.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana mbali mbali .

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana wazalendo waliofanya matembezi ya Uzalendo.

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Taifa baada ya kupokea maandamano ya vijana wazalendo katika ukumbi wa PTA, Dar-es-Salaam.