Unknown Unknown Author
Title: TAZAMA PICHA YA ACCIDENT MBAYA ILIYOUA BABA NA KUJERUHI MTOTO MAENEO YA NANENANE MBEYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtu mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili  T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katik...



Mtu mmoja ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari lenye namba za usajili  T. 495 ALM aina ya Nissan Pick Up amefariki dunia katika  ajali mbaya huku mtoto wake akijeruhiwa vibaya maeneo ya Nane Nane  hapa jijini Mbeya usiku wa kuamkia jana Septemba 01,2014 majira ya saa saba za usiku.

 Dereva huyo aliyefariki dunia amefahamika kwa jina la Boniface Mwasoba alifariki dunia baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka katika maeneo hayo ya Nane Nane ajali iliyopelekea pia kujeruhiwa kwa mtoto wake anayefahamika kwa jina la Willy Boniface Mwasoba mwenye miaka 7 na mwanafunzi wa shule ya msingi Mkapa na amelazwa katika hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.

Mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika japokuwa polisi bado wanaendelea na uchunguzi ili kubaini, lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto kwa kuzingata sheria na alama za usalama wa barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
CHANZO:KIBONAJORO

02 Sep 2014

About Author

Advertisement

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top