Unknown Unknown Author
Title: 22 NOVEMBA:NIME TIMIZA MIAKA KADHAA!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Unapo anza kuona aibu kutaja Umri wako sahihi mbele za watu! Ukaanza Kuificha ficha ni wazi kwamba umesha tambua kuwa Hakuna Mahusiano Kat...
Unapo anza kuona aibu kutaja Umri wako sahihi mbele za watu! Ukaanza Kuificha ficha ni wazi kwamba umesha tambua kuwa Hakuna Mahusiano Kati ya Miaka yako ya kuwepo Duniani na Hatua Ulizo piga! Ndiyo maana Unajaribu kuuficha ukweli,Nafsi ina kusuta Unaogopa Kusema Kweli Kweli ambayo itakuweka Huru.Wengine Hufikia hatua wakasema Laiti Ninge kuwa Kijana.....

Katika Maisha kuna kipindi Lazima Utafute Pesa kwa bidii zako Zote,Hasa kwa sababu wa Tanzania tulio wengi tume jijengea utamaduni wa kutafuta pesa.Yaani Pesa ndiyo lengo kuu la Maisha yetu... na Sio Maisha tena.
Ndio maana wengi wetu hata katika maziwa fresh ya kuwa Uzia Wateja Wetu Tuna ongeza Maji,ama kwenye kila kilo moja ya nyama za mteja tuna mwibia robo.Kwasababu Tuna Tafuta Pesa Wala Hatu fanyi Maisha maisha ambayo ndiyo lengo kuu.
Sijui Umri sahihi wa kila binadam kuanza Kutafuta pesa,yaani ukitimiza miaka mingapi ndo uanze rasmi kutafuta pesa.Nasema sijui kwasababu kuna watu wame anza kuingiza fedha tangu wakiwa matumboni mwa mama zao,Siku wana Zaliwa mpaka siku wana kufa.Kwahiyo mimi nina Amina Umri kamili wa lini mwana damu aanze kutafua pesa nina amini haujulikani.
Mfano kuna Rekodi kuwa Pele alianza kiuchezea Timu yake ya Taifa kwa mara ya kwanza kombe la Dunia akiwa na Umri na Miaka 17 tu! Yaani umri wa Miaka yangu Toa miaka Kumi.
Japo kwa utamaduni wetu wa ki Tanzania unapo timiza miaka miaka 18(Kama Haupo Shuleni),Inatakiwa mzazi aku ondoe kwenye bajeti zake(akutoe kwenye pochi yake ama Mfukoni).Yaaani uache kumtemtegemea Mzazi;Ujitegemee! Kama ina wezekana utoke nyumbani kwa wazazi na wewe ukatafute vyako.
Tiari tume ona umri wa kutafuta pesa ni upi! Lakini swali  lina kuja,Je,Umri wa kuacha kutafuta pesa ni upi? Yaani ule umri wa kuacha nita nunua unga niki pata mshahara au Nita enda Kutibiwa nikipokea mshahara au Subiri Mshahara Utoke ntakulipa deni lako.Kweli kabisa kama binadamu hatuishi milele lazima pia tujipangie ratiba ya maisha yetu vema ili tuje lini,Tuishi vipi?
Kama katiba yetu inatambua kuwa miaka 18 kijana lazima aanze  kujitegemea rasmi,Naamini wali panga umri huo wakijua wazi kuwa kijana anakuwa amepevuka kimwili na kiakili na  pia kwa kutumia mfumo wa jamii husika na malezi ya wazazi wake.
Kwakua kuna kipindi kitafika miili yetu ita fika ukomo;Nguvu zita pungua(kwani nguvu ndio mtaji wa maskini).Lazima tuweke ukomo wa kuzitumikia pesa;Na kuanzia hapo tuanze kuzituma pesa tulizo zitafuta miaka kadhaa zitu tumikie pia.
Kwa kawaida unapo kuwa mtumishi  katika sekta yeyote ile kuna umri kustaafu.Umri ambao watumishi walio wengi wangetamani waufikie ili wapewe kiinua mgongo chao huku waki pumzika au kufanya kazi kwa mkataba.Umri ulio zoeleka zaidi ni miaka 55 hadi 60,Huu ndio umri ambao wengi huwa Tuna Pumzika.
Tukiachana na Uvumi kuwa maisha yana anza ukitimiza miaka 40.Kiukweli maisha ya kuishi hapa duniani ni mapupi sana,Tuna muda mfupi ambao lazima tufanye mambo mengi sana kwa faida ya vizazi vijavyo Siku hizi hasa kwenye mazingira yetu ya Ki Tanzania Kijana kuufikia Umri wa kiinua mngongo imekuwa ni kama ni kwa neema tu na Rehema za Mwenyezi MUNGU.
Kuna vikwazo vingi vinavyo katiza maisha/Uhai wetu Ukikwepa ajali kuna magonjwa,Ukikwepa Magonjwa kuna Vibaka,yaani ni kama maisha ya digi digi kabti kati ya mbwa mwitu ama simba wenye njaa kali.
Kutokana na wingi wa vikwazo katika kutimiza umri wa kiinua mgongo kama tulivo ona hapo.Rai yangu kwa vijana ifike kipindi tuilete hiyo miaka isogee mpaka miaka 45 badala ya ile 60 iliyozoeleka,Akilini mwetu.Tujiwekee ukomo wa kutafuta pesa yaani ije ifike kipindi tuseme sasa na wewe pesa Tafuta pesa.NTuiishi kwa mazoea sasa ni wakati muafaka wa pesa ulizo zitafuta (Hata kama ni kidogo) kuzi tuma zika tafute wenzake.
Miaka 45 sio haba ni wazi kuwa kama pesa utakuwa ume tafuta kwa wastani ni miaka zaidi ya Ishirini kama utakuwa ulianza kujiwekekea akiba ukiwa na miaka 25,Hivyo ni wakati wa kuituma pesa yako nayo! Kwani hakuna kipimo cha zipi ni pesa nyingi au chache,Chache kwako ni nyingi kwa wengine,Ume ona eeh.
Wahenga walisema kandege kaliko kiganjani mwako ni bora zaidi kuliko lile kundi kubwa la ndege lililo kule mstuni.Wale wengi kule ni wamstuni lakini huyo mmoja ndiye mali yako wewe! Ndege huyo kama utamtunza anaijua vema milio ya kuwaita wale wengi,ili waje hapo andaa mazingira ili watakapo fika nao watamani kjenga kiota.
Maelezo hapo juu ni mfano tu wa jinsi ya kuanza na hatua moja ili ufike tatu.Japo rai yangu sio sheria eti kwamba usipo ifuata utafungwa, lahasha.Wengine kuleni bata(Ujana maji yamoto) Ila kumbukeni Tip Top waliimba kua "Bata bila kazi ni sawa na kesi bila dhamana.Kama ukioipereka pesa yako yote unayo itafuta Bar na una amini ipo siku itarudisha faida peleka.Maisha ni yako chaguo ni lako.Mimi huwa nina sema Kupanga ni kuchagua.Yale unayo yachagua kuya fanya ndo ueyapanga kwani uliyo yapanga utayachagua.
Nimalize kwa kutoa Shukrani za dhati kwa wale wote mlio nipa pongezi Siku yanu ya Kuzaliwa.Nasema Asanteni sana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top