Unknown Unknown Author
Title: SALAAM ZANGU LEO KWA WIZARA YA ELIMU:TUFUTE UJINGA,TUSIFUTE ZERO!!!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mmh;kuna wakati utamu wa kauli mbiu za kiprpaganda zina weza zika kufanya ukapoteza kabisa uwezo wako wa KUFIKRI.Ukajikuta na wewe ni sehemu...
Mmh;kuna wakati utamu wa kauli mbiu za kiprpaganda zina weza zika kufanya ukapoteza kabisa uwezo wako wa KUFIKRI.Ukajikuta na wewe ni sehemu ya waeneza propaganda na kauli mbiu za reja reja kwa masrahi ya kikundi flani cha watu wenye malengo yao binafsi.
Leo hawa wenzetu wa idara ya Elimu wame amua kutuaminisha kuwa zero ya kwenye karatasi ikisha futwa kwa watahiniwa basi matatizo ya kitaaluma kwa watahiniwa wetu yatakuwa yame pata Suluhu ya kudumu.Kwmba ziro ikisha futwa kwenye cheti cha kila mtahiniwa wanafunzi wasio jua kusoma na kuandika lakini waka chaguliwa kuingia sekondari itakuwa sio tatizo tena,Nao wale wanao chora mazombi kwenye karatasi ya kujibia mtihani watafitika,Wanao andika ludha za kejeli,vijembe na matusi wata okoka.
Je, hayo ndiyo matokeo makubwa sasa? hivi kipi bora kufuta zero ya kwenye cheti ama kuufuta Ujinga vichwani mwa watahiniwa? Na je,Mtihani wa Taifa ndio kipimo pekee cha kuupima  Ufahamu wa Mtahiniwa?
Rai yangu kwa wadau wote wa Elimu nina waomba Tufute UJINGA kwa watahiniwa;Tusi ifute ziro ya kwenye cheti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top