KIKAO CHA KAMATI KUU CHADEMA KESHO 03,JANUARI;2014!
Taarifa Iliyo Tolewa na Mkurugenzi wa Habari CHADEMA Ndg John Mnyika kwa vyombo vya habari ina someka hivi:-
"Nikweli kutakuwa na mkutano maalum wa kamati kuu ya Chama kesho Tarehe 03,Januari 2014 JIJINI Dar es salaam agenda kuu katika kikao hicho ni tatu.
Mosi.Kupokea taaifa kuhusu mchakato na madhumuni ya Mabadiliko ya Katiba
Pili:Kupokea utetezi (wa Mdomo) wa wana chama watatu kuhusu tuhuma mbali mbali zilizo elekezwa kwao.
-Wana chama hao walisha julishwa makosa yao kwa maandishi na waka wasirisha utetezi wao kwa mandishi.Watatakiwa kwenye kikao kwa kuzingatia matakwa ya kanuni ya 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya kujielez mbele ya kikao kinacho husika.
Tatu:Mpango kazi kwa mwaka 2014
-Mpango kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa mpango mkakati makini wa oganaizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama na Taifa.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Mwasiriano
MJUMBE sr
MBEYA

Post a Comment