POLISI NCHINI AFRIKA KUSINI:ALIYE KUWA MKUU WA IDARA YA UJASUSI WA RWANDA PATRICK KAREGEYA AMEPATIKANA AMEAGA DUNIA KATIKA HOTEL,MJINI JOHANNESBURG!
Polisi nchini Afrika Kusini Wamesema kuwa aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi wa Rwanda Patrick Karegeya amepatikana ameaga dunia katika Hotel,Mjini Johannesburg.
Bwana Karegeya amekuwa akiishi uhamishoni kwa muda wa miaka sita.Karegeya alipokonywa cheocha Kanali baada ya kutofautiana na Mshirika wake wa Zamani Paul Kagame ambaye alimshutumu kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi Mjini Kigali,Rwanda.Katika taarifa iliyo tumwa kwa vyombo vya Habari na chama cha Upinzani cha Rwanda Congress(R.N.C),Imesema kuwa Karegeya alinyongwa ndani ya chumba chake.
Hata hivyo mamlaka nchini Afrika Kusini haija thibitisha.
chanzo:bbc
MJUMBE sr
MBEYA

Post a Comment