Pwani. Mathayo Torongey ndiye
mgombea mteule wa nafasi ya ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze wilayani
Bagamoyo mkoani Pwani.Torongey ni mkazi wa Kata ya Ubena, Chalinze
wilayani Bagamoyo na ni mtoto wa mwisho wa kiume katika familia ya
watoto watano wa mama Maria Torongey ambaye alizaliwa mwaka 1978 katika
Kijiji cha Mlenge Kata ya Ubena Hata hivyo kwa mila za Kimasai, mgombea huyo pia
ni mtoto wa 17 kwa upande wa baba mzazi Mzee Mng’unda Ole Torongey
ambaye ni Mkazi wa Mlenge Kata ya Ubena kwa kuwa mzee huyo katika maisha
yake amefuata mila na desturi za kabila la Kimasai ambayo inaruhusu
kuoa mke zaidi ya mmoja.Akizungumzia historia yake, Torongey anadai
amezaliwa vichakani kwa msaada wa wakunga wa jadi kwa sababu hakukuwapo
na vituo vya afya vilivyokuwa vikitoa huduma ya uzazi wakati huo
kwenye maeneo ya vijijiniKutokana na utamaduni wa kabila la Kimasai,
Torongey akiwa mdogo mwenye miaka minane, alikuwa akijihusisha zaidi na
ufugaji kwa kushirikiana na familia yake akiwamo baba, kaka na hata mama
yake mzazi.Akiwa na umri huo, Torongey anaelezea kuanza
darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mvomero, Kata ya Turiani na
baadaye alifanikiwa kujiunga na Sekondari ya Mvomero mwaka 1997 na
kuhitimu elimu ya kidato cha nne mwaka 2000 shuleni hapo.Baada ya kuhitimu masomo ya sekondari, Torongey
alijikita katika ufugaji na aliweza kumiliki zaidi ya mifugo 100
kijijini kwao, mtaji ambao aliupata kutoka kwa wazazi wake .Hata hivyo mwaka 2006 alianza kupanuka kibiashara
na kufungua maduka mawili ya kuuza nyama maarufu kama bucha kijijini
hapo na miaka mitatu baadaye alifungua mengine katika maeneo tofauti
mkoani Pwani ikiwamo Chalinze ambako alifungua bucha sita na Bagamoyo
mjini bucha tatu.Pamoja na kujikita katika shughuli hizo, mgombea
huyo ni baba wa familia ya watoto wawili na mke mmoja ambaye mpaka sasa
anaishi katika Kata ya Ubena, Chalinze.Kuhusu masuala ya siasa, Torongey anasema alianza
kupenda siasa mwaka 1999 baada ya kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere .Alisema alivutiwa na siasa kutokana na utaratibu
katika majukwaa ya kisiasa zlizoonyeshwa katika vyombo vya habari
mbalimbali vya televisheni, ikiwamo misemo yake ya kutopenda ubaguzi,
ukabila na msisitizo wa kuwapo amani, umoja na mshikamano.Hamasa hiyo ilimfanya kugombea nafasi ya
mwenyekiti wa tawi kupitia Chadema mwaka 2010 ambapo alifanikiwa
kuchaguliwa kuwa kiongozi katika Kata ya Sinza B, Dar es Salaam mwaka
huo.Chanzo:Mwananchi
Mjumbe Jr
Mjumbe Jr
Post a Comment