Unknown Unknown Author
Title: NDEGE YA MALAYSIA ILIYOTOWEKA BADO HAIJAPATIKANA,JUHUDI ZA KUITAFUTA ZAENDELEA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ndege za Vietnam zikiendelea na shughuli ya kutafuta ndege ya Malaysia ...

Ndege za Vietnam zikiendelea na shughuli ya kutafuta ndege ya Malaysia

Wakati juhudi za kuisaka ndege iliyopotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Malaysia kuelekea Uchina zikiendelea, ndege moja ya Vietnam imeripoti kuwa imeona kitu kinachofanana na mlango wa ndege kwenye ufuo wa bahari ya Kusini mwa Uchina kwenye mwambao wa taifa hilo.
Hata hivyo hakuna thibitisho kuwa mlango huo ni wa ndege iliyopotea ya Malaysia, iliyokuwa na abiria mia mbili na thelathini na tisa.
Uchunguzi kuhusiana na kilichosababisha kupotea kwa ndege hiyo mapema siku ya Jumamosi, inawalenga abiria wawili wanaodaiwa kuwemo ndani ya ndege hiyo, waliotumia paspoti iliyoibiwa.
Stakabadhi hizo mbili za kusafiria kutoka Italia na nyingine Australia inaaminika kuibwa nchini Thailand.
Idara ya polisi ya Kimataifa, Interpol, inasema kuwa ni mapema mno kuhusisha pasi zilizoibwa na kutoweka kwa ndege hiyo.
Na huku kushughuli za kuisaka ndege hiyo zikiendelea, Msemaji wa shirika la ndege la Malysia amewaambia jamaa ya watu waliokuwemo katika ndege hiyo, kujiandaa kwa taarifa mbaya.
Maafisa wa Idara ya usafiri wa ndege wa Malaysia

Amesema kufikia sasa hakuna mawasiliano yoyote na ndege hiyo masaa 30 sasa tangu itoweke.
Wakuu wa Malysia wanasema jumla ya meli 30 na ndege 44 kutoka mataifa tisa tofauti duniani, yamejiunga katika shughuli za kuitafuta ndege hiyo.
Kamanda William Marks wa kikosi cha saba cha jeshi la wanamaji la Marekani, ametuma ndege aina ya USS Pinckney kusaidia katika usakaji huo.
''Jambo la kwanza kufanywa ni kukadiria mahala na kwa sasa tunalenga mawasiliano ya mwisho kutoka kwa ndege hiyo kabla ya kutoweka na mawasiliano ya rada. Kutoka hapo tunahesabu mwendo kasi ya upepo na mawimbi. Kutoka hapo tunagawanya na eneo na tunatafuta kutumia kila kifaa tuliyonayo- na hiyo siyo tu kutumia vifaa kutoka Marekani lakini pia kutumia meli na anga kutoka mataifa mengine ya dunia." Alisema kamanda huyo.
Ameonya kuwa shughuli hiyo ya kutafuta ndege hiyo inakumbwa na changamoto nyingi.
Chanzo:BBC SWAHILI
Na Mjumbe Jr
Mbozi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top