Unknown Unknown Author
Title: SAED KUBENEA:NAYE ASHANGAZWA NA HOTUBA YA MHE.RAIS! IME MWACHIA MASWALI MENGI KULIKO MAJIBU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HOJA ZAKE AMEZIJENGA ZAIDI KATIKA MASWALI YAFUATAYO # kama tume ya Rais ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji JOSEPH SINDE WARIOBA hikuw...
HOJA ZAKE AMEZIJENGA ZAIDI KATIKA MASWALI YAFUATAYO

# kama tume ya Rais ya mabadiliko ya katiba chini ya Jaji JOSEPH SINDE WARIOBA hikuwa sahihi mbona ilikuhusisha kila hatua waliyofikia,na hukusema chochote zaidi ya kuwaamuru waendeleee???

‪#‎Na‬ kama ofisi ya waziri mkuu iliyochini yako ilitoa maoni yanayofanana na yaliyopo kwenye tume ya mabadiliko ya katiba " yaani serikali 3" unawezaje kuyakataa kiasi hicho, au unataka kutuambia kuwa taasisi za serikali pia zilikusaliti? ama hazijui chochote kuhusu changamoto za muungano???

‪#‎Pia‬ kama mshauri mkuu wa Tume kuhusu mapato ya serikali hasa kwenye ,muundo wa muungano wa serikali 3 ni mamlaka ya mapato Tanzania yaani "TRA" ambao ni wataalamu wetu kwenye mambo ya mapato ,wewe mh,umeshauriwa na akina nani kuhusu mapato ?? na kama ni hao hao TRA kwanini wamekupa ushauri tofauti na Walioipa tume??? ukizingatia umeonyesha hofu kubwa kwenye suala la mapato ya serikali3??

#Na kama wewe na chama chako kama ulivyosema jana mnaamini serikali 2 mpaka hatua hii ambayo muda wa kutoa maoni kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba umepita hamunoni mnaingilia maoni ya wananchi kwa kutumia nafasi yenu kuwa madarakani???

‪#‎Lakini‬ pia jana ulionyesha hofu kuwa inawezekana kwa muundo wa serikali 3 wanajeshi na polisi kuasi labda kwasababu wanadai mishahara yao au posho zao, ukiwa umesahau kuwa Jeshi la polisi linamadai makubwa kuliko walimu kwenye muungano huu wa serikali 2 lakini hawajapindua. eti mh unasemaje kuhusu hili???

# Na kwanini jana umekwenda kulihutubia bunge kama mjumbe wa bunge maalumu la katiba na sio kufungua bunge kama tulivyotaarifiwa kwani ulikwenda kuichambua Rasimu,na kuna umuhimu gani Bunge kuwepo kama umeshaelekeza mambo yanavyopaswa kufanyika?? si waondoke ukae na watu wachache ikulu mtengeneze katiba tuepushe gharama zisizo na maana ??

‪#‎Mwisho‬ umetutisha kuwa serikali 3 zinaweza kusababisha jeshi kupindua na wanajeshi kuongoza nchi na baadae kuvua magwanda na kugombea Urais, umesahau kuwa wewe pia ni Luteni wa jeshi uliyevua magwanda na kugombea Urais ??? na tena kwa mujibu wa katiba yetu wewe ni mkuu wa vikosi vyote nchini??? tatizo liko wapi?? mpaka ututishe???


Leo Kwenye Kipindi Cha Tuongee Asubuhi
Star Tv



MJUMBE sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top