Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva akiongea na
vyombo vya Habari leo Mkoani Iringa akifafanua juu ya Daftari la Kudumu
la Wapiga kura Jimbo la Kalenga.
Baada ya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukutana na Viongozi wa Siasa vinavyoshiriki
Uchaguzi wa Ubunge wa Jimbo la Kalenga mnamo tarehe 12 mach 2014, na
kutoa taarifa kuhusu maadalizi ya Uchaguzi katika jimbo hilo.
Vyama vya
Siasa katika mkutano huo viliarifu kama ilivyokuwa katika chaguzi ndugo
zilizopita, daftari la kudumu la wapiga kura litakalo tumika katika
uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kalenga ni lile lililotumika katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2010.
Kutokana
na hoja hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa ufafanuzi kuhusu daftari
la kudumu la wapiga kura litakalotumika katika uchaguzi wa Ubunge Jimbo
la Kalenga utakaofanyika 16 mach 2014.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji St. Damian Lubuva amesema kuwa,
Tume kwa mamlaka iliyopew na Sheria na Kanuni za Uchaguzi imekuwa
ikipitia na kuhakiki Daftari la kudumu la Wapiga kura lililotumika
katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 kwa dhumuni la kuondoa kasoro ndogo ndogo
zilizokuwepo katka daftari hilo.
Jaji
St.Lubuva amesema, Kasoro hizo ni kuwaondoa wapiga kura ambao taarifa
zao zinatokea kwenye daftari zaidi ya mara moja pamoja na kuweka majina
ya kupiga kura ambao walijiandikisha hapo awali na wana kadi za kupiga
kura ambapo kwasababu mbalimbali za kimfumo, majina yao hayakutokea
kwenye daftari lililotumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Ameongeza
kuwa, kilichofanyika ni uhakiki wa daftari hilo ili kuwa sahihi zaidi
na kuhakikisha kila aliyeandikishwa awali na kupewa kadi ya kupiga kura
anatumia haki yake ya kupiga kura, ili kuondokana na malalamiko ya
kushindwa kupiga kura kwa sababau ya kukosekana jina la mpiga kura
katika kaftari hilo.
Aidha amesema, idadi ya wapiga kura ni 71,957 pamoja na vituo vya kupiga kura 216 vilivyopo katika jimbo la Kalenga.
Jaji
St.Lubuva ametoaonyo rai wa vyama vya siasa kufuata taratibu na sheria
walizowekewa ili kuchaguzi ufanyike kwa hali ya utulivu na haki pasipo
uvunjifu wa amani.
Hata
hivyo, amesema uchaguzi mgogo wa ubunge utafanyika tarehe 16 machi 2014
katika Jimbo la kalenga na kuagiza vyama vya siasa kutii agizo la kukoma
kwa kampeni zao ifikapo tarehe 15 machi 2014 majira ya saa 12 jioni.
MJUMBE Sr
Post a Comment