Unknown Unknown Author
Title: BABA AUA MTOTO WAKE WA MIAKA MITATU KWA KUMPIGA NGUMI HUKO MBEYA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KATIKA TUKIO LA KWANZA:  MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUP...
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

 MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO (03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK  NJOJO (23) MKAZI WA ISISI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YAWILAYA MBARALI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WAPOLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.

KATIKA TUKIO LA PILI:

 MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 4– 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO  MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA,BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI
KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
                                                    
Signed by:
 
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top