Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura.
Wakazi wawili wa eneo la Kiluvya Gogoni, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, Barnabas Swai (33), Pendo Mchaki (26) na Lugano Kalinga, wamejeruhiwa kutokana na kipigo cha watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWT) na mmoja wao akilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Wakazi wawili wa eneo la Kiluvya Gogoni, Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar es Salaam, Barnabas Swai (33), Pendo Mchaki (26) na Lugano Kalinga, wamejeruhiwa kutokana na kipigo cha watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, (JWT) na mmoja wao akilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Tukio hilo lilitokea juzi na inadaiwa kuwa chanzo
cha kipigo hicho ni mmoja wa maofisa wa jeshi hilo aliyefika kwenye baa
na mkewe na baadaye ulizuka ugomvi uliodaiwa kuzuka kutokana na mke wa
ofisa huyo kudhulumiwa nyama choma, lakini walizidiwa nguvu na kupigwa.
Habari zinasema baada ya tafrani kutokea ofisa
huyo wa jeshi aliondoka, baadaye walifika askari na kuanza kupiga watu
ovyo njiani, kwenye maduka na baa za eneo hilo na kujeruhi baadhi ya
watu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,
Camilius Wambura jana aliliambia gazeti hili kuwa hajapata taarifa za
tukio hilo.
“Ofisini kwangu sina taarifa kama hiyo, nashukuru
kwa kunifahamisha nitazifanyia kazi,” alisema Wambura. Msemaji wa Jeshi
la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Eric Komba hakupatikana
kuzungumzia tukio hilo, baada ya simu yake kutokuwa hewani.
Barnabas inaelezwa amepata majeraha katika maeneo
mbalimbali ya mwili na damu imevujia kwenye mapafu, wakati Pendo ambaye
ni mkewe alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Tumbi na kuruhusiwa.
Hata hivyo, akizungumza kwa shida kutokana na
maumivu katika Wodi namba 5A, Hospitali ya Mwananyamala alikolazwa, Swai
alisimulia kwamba yeye na mkewe walikuwa kwenye Baa ya Gogoni Inn na
waliona watu wanakimbia ovyo eneo hilo na nao walipoamua kukimbia,
walivamiwa na wanaodhania kuwa ni askari wa JWTZ kutokana na kuvaa
suruali za jeshi na mashati ya kiraia.
Alisema kuwa walipigwa kwa kutumia mikanda ya
jeshi iliyokuwa na vyuma, virungu na vitu vya ncha kali na wakati
akipigwa alitobolewa eneo la mgongoni na kupata maumivu makali huku
akipumua kwa shida.
Hivyo yeye na majeruhi wengine walipelekwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kabla ya kuhamishiwa Mwananyamala.
“Walinifanyia upasuaji na kuniweka mpira wa kutoa
damu iliyoanza kuganda, lakini kwa sasa naendelea vizuri, ingawa nahisi
maumivu makali sehemu ya mgongoni,” alisema Swai huku akiomba apatiwe
dawa ya maumivu kutokana na maumivu makali anayoyahisi.
Daktari wa zamu katika wodi namba 5A, katika
Hospitali ya Mwananyama Daktari Brian Minja alisema: “Kulingana na faili
lake, ‘mgonjwa huyo alipokewa usiku na daktari mwingine, inaonyesha
alikuwa na tatizo la kupumua kutokana na damu kuvujia kwenye mapafu.
Karibu lita mbili za damu ilitolewa.”
Naye Upendo Swai alisema kwamba mume wake
aliumizwa kwa sababu alikuwa akimkinga yeye kuzuia asipigwe zaidi na
askari hao na kufafanua kwamba katika kipigo hicho, yeye aliumizwa usoni
kwa kukanyagwa na viatu pamoja na kuchomwa na kitu chenye ncha kali
eneo la kwapani.
Kwa upande wake Lugano Kalinga ambaye ni mkazi wa eneo hilo,
alisema alipigwa na askari hao, ingawa alifanikiwa kukimbia na hakupata
majeraha makubwa.
Alisema kilichosababisha wapate kipigo hicho ni
ofisa mmoja wa jeshi kugombana na muuza chipsi baada ya kukataa kumlipa
fedha zake, ndipo kijana huyo alipigana na ofisa huyo pamoja na mkewe
lakini aliwazidi nguvu.
“Baada ya kutoka pale, ndiyo maaskari wakavamia
eneo hilo na kuanza kumpiga kila waliyemwona, hali inayoonekana ni
kupata maelekezo kutoka kwa huyo ofisa aliyepigana kwenye baa ya
Kiluvya, ”alisema Kalinga.
Post a Comment