Unknown Unknown Author
Title: KESI YA PONDA NGOMA NZITO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, imeendelea kusota mahakamani hadi hapo ...

ponda_249da.jpg

Kesi inayomkabili Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya ya Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda, imeendelea kusota mahakamani hadi hapo jalada lake litakaporudishwa toka Mahakama Kuu.Akiahirisha kesi hiyo jana hadi Aprili 16, Hakimu Mkazi Mkoani Morogoro, Marry Moyo, aliitaka Idara ya Upelelezi kufuatilia jalada la mtuhumiwa huyo Mahakama Kuu ili kesi ianze kusikilizwa.
Akionekana mwenye afya njema, Sheikh Ponda anayetetewa na wakili Batheromeo Tharimo, alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi licha ya kutokuwepo umati mkubwa wa wafuasi wake.
Mara baada ya kufikishwa mahakamani hapo, wakili Tharimo alidai kuwa amewasiliana na wakili mwenzake, Juma Nassoro, ambaye naye anamtetea Sheikh Ponda, na kwamba kuna ombi waliliwasilisha Mahakama Kuu la kutaka shauri hilo kutoendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.
Chanzo:Mjengwa
Mjumbe jr
Read more...

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top