Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifungua kongamano hilo
ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mada juu ya fursa za uwekezaji nchini
Tanzania katika sekta za mafuta, gesi ikiwa ni pamoja na madini.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akifungua kongamano hilo.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto)
akisalimiana na mmoja wa wajumbe anayewakilisha wafanyabiashara kabla ya
kufungua kongamano la mafuta na gesi linaloendelea huko Ujerumani kama
moja ya maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Mtaalamu
kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) Bi Venosa Ngowi
(kulia) akimweleza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(mwenye suti nyeusi) shughuli zinazofanywa na shirika hilo kwenye
maonesho yanayoendelea huko Berlin, Ujerumani. Pembeni ya Waziri ni
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.
Mtaalamu
kutoka Wakala wa Jiolojia Nchini (GST) Bi. Augustina Rutaihwa akitoa
maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
(katikati) juu ya shughuli zinazofanywa na wakala huo. Kushoto mwa
Waziri ni Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo.
Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa kongamano hilo.
Post a Comment