"UNATAKA KUSIKILIZA LIPI;NIKWAMBIE UKWELI au UNATAMANI NIKUDANGANYE?" Hayo Maneno yapo Kwenye
Moja ya Mahojiano ya Aliye wahi kuwa Mwigizaji maarufu nchini Marehemu
Steven Kanumba(RIP).Kweli kuna
kipindi Kabla hauja amua kumweleza mtu jambo analo taka kujua kutoka
kwako Lazima Umusome kwanza yeye anataka nini? Na ikibidi umuulize...
Anataka Kusikiliza Uongo au Ukweli? Marafiki Zangu walio wengi wanapenda
kusikiliza Uongo ukiwadanganya ndio watakupenda zaidi.Leo ni Miaka
50 Tangu Wazanzibar Waungane na Tanganyika na hata kuzaliwa nchi moja
inayo itwa TANZANIA,Nchi ambayo wengi ndiyo imetulea.Kume kuwa na
mvutano wa Muundo wa Serikari katika Bunge Maalumu la katiba wa ama
kufuata Maoni ya wananchi(Haya yamepewa jina ni Maoni ya wachache au
Maoni ya Warioba) yanayo pendekeza muundo wa Serikari Tatu na Maoni ya
Wajumbe Walio Wengi ndani ya Bunge la katiba Msimamo wao Ukisimamiwa
Rais wa nchi pia! wao wana sisitiza kuwa pamoja na Changamoto zinazo
zikabili Serikari mbili,lakini zina weza kutatulika na
kuzungumzika,hivyo hakuna umuhimu wa kuongeza mzigo zaidi wa Serikari ya
tatu.Nahapa kwa Utashi wangu hawa wanao ogopa
mabadiliko(Wahafidhina) wana kuja na hoja za kutishia wananchi kuwa kama
Serikari zikiwa Tatu iyo ya tatu itakosa nguvu na hata inaweza
kupelekea jeshi kuasi na kushika hatamu kwa siku zijazo! Hapa ndipo
wengi wame ibuka kuanza kumshambulia Mzee Jaji Joseph Warioba na kusema
Alianzaje kukubali haya maoni ya muundo wa Serikari tatu? Hapa Maoni ya
wana nchi yamegeuzwa jina na yana itwa maoni ya Warioba! Kun a uvumi wa
Vitisho vingi kwa raia kuhusu muundo wa Serikari tatu kuliko hoja za
msingi zilizo tolewa na tume.Na hii katika ile Elimu ya Mantiki
wataalamu wana ita "ad hominem" yaani badala ya mtu kujibu hoja za
Mhusika wana anza kumushambulia na hata ikibidi kumubatiza majina
mabaya.Wajumbe wengi na rais wa jamuhuri ya muungano wao wana
hitimisha kwa kupigia chapuo muundo wa serikari Mbili tu,katika hili wao
wana sisitiza kuwa ni ama serikali mbili au kama hamtaki tuikabidhi
nchi jeshi! Hili nalo katika Elimu ya mantiki wataalamu wanalifafanua
kama "a fallacy of two dilema" yaani baada ya wewe kutoa hoja,anaye
ijibu hoja yako ana kupa jibu kwa machaguo mawili pekee hapa ndio kuna
msemo ule wa Ukitaka usuke au unyoe! Lakini Ukijiuliza hivi kuna mitindo
miwili tu ya usukuaji nywele? Hakuna Afro,Hakuna Rasta? hakuna Viduku
na mitindo mingine? Hapo ndipo tuna sema hoja si kuchagulia muhusika
majibu unayo tamani kuyasikiliza wewe,Mwache aje na Majibu yake na
msimamo wake huenda hata wewe kuna jambo utajifunza.Kuna wanao
tetea muundo wa Serikari mbili kwa kuhusianisha na Umri wa wengi walio
zaliwa baada ya muungano na kuhitimisha kirahisi kuwa kwasababu Umri wa
Muundo wa serikari mbili ni mkubwa kuliko hao wachache wanao dai muundo
wa Serikari tatu basi waulinde muundo ulio walea;Hii hoja nayo haina
mashiko kwani,Sisi(Binadamu) ndio tulio chagua muundo wa serikari
amabayo kwa Muda na wakati wake Tuliamini inatufaa na Sio muundo wa
Serikari ulio tuchagua sisi! yaani Hakikuundwa kijiko ndio vikaumbwa
vidole bali viliumbwa Vidole ndio kikaundwa kijiko! Katika Hili la
Kaluli yangu kuhusu muundo wa Serikari ninayo itamani iwepo;lisi
Husianshwe na Imani yangu,Itikadi yoyote ile wala Shughuli yngu yoyote
ile niifanyayo.Huo ni Mtazamo wangu na huo ndio ukweli wa Ninacho
Kitamani mimi,Vinginevyo Nitakuwa nimekudanganya.
SERIKARI TATU NDIO MUUNDO PEKEE Utakao Kidhi mahitaji ya Muda na Wakati Tulio nao.
Elasto Mbella
Elasto Mbella
MBEYA
Post a Comment