Unknown Unknown Author
Title: PISTORIUS KUDADISIWA MARA YA MWISHO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mahakama ilibidi isitishe kikao kila Pistorius alipozidiwa na hisia Mwanariadha huyo aliyekatwa miguu yote miwi...











Mahakama ilibidi isitishe kikao kila Pistorius alipozidiwa na hisia
Mwanariadha huyo aliyekatwa miguu yote miwili anakana kutekeleza mauaji hayo akisisitiza kwamba alidhani Bi Steenkamp ni mvamizi nyumbani mwake.

Kabla ya kuanza kusikizwa kesi hiyo, mwendesha mashtaka Gerrie Nel alisema kuwa alitumai kumaliza kumhoji mwanariadha huyo siku ya Jumanne.Anakabiliwa na kifungo cha kati ya miaka 25 au maisha gerezani, iwapo atapatikana na makosa ya mauaji ya kupangwa.
Alimuomba Jaji Masipa aahirishe kesi wakati wa mapumziko ya pasaka hadi tarehe 5 Mei.
Ameeeleza kwamba mawakili wenzake wanakabiliwa na kesi nyengine 'nzito zaidi' wanazostahili kuzishughulikia pamoja na 'masuala ya kibinafsi'.
Ombi hilo liliungwa mkono na upande wa utetezi, uliosema kwamba kesi hiyo inapaswa kumalizika tarehe 16 Mei kama ilivyopangwa. Jaji alisema atatoa hukumu yake ya ombi hilo siku ya Jumatano.
Nel anajulikana kwa kutishia watu anapowahoji,
Siku ya Jumatatu, Bwana Nel alipendekeza kwamba Pistorius anajifanya kuzidiwa na hisia kuficha matatizo anayopata kujibu masuali mazito anayoulizwa.
Jaji Thokozile Masipa alisitisha kwa muda kesi hiyo mara mbili siku ya Jumatatu baada ya Pistorius kuanza kulia.
Muda mfupi kabla kesi kumalizika kwa siku, Nel alisema: " unazidiwa na hisia sasa kwa sababu unaudhika, kutokana na kuwa ushahidi wako huenda si wa kweli."
Mwendesha mashtaka huyo anayejulikana kwa mtindo wake wa kutishia watu anapowahoji, baadye alimuuliza Pistorius: " Hautumii hisia zako kukwepa kujibu maswali?"
Pistorius alisema akili yake haikumanika kama inavyostahili wakati wa ufyetuaji risasi huo.
Oscar PIstorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
Awali, kwa mara nyengine Nel alimdadisi kwa uzito Pistorius kuhusu wakati alipompiga Bi Steenkamp risasi.
Mwanariadha huyo alisisitiza kwamba hakuna na nia ya kumuua mtu yoyote, alisema: "Nilifyetua risasi kutokana na uoga."
Nel baadaye alisema kwamba Pistorius alibadili ushahidi wake kutoka kusema alikuwa akijikinga na hadi kusema kwamba alifyetua risasi kwa makosa.
Pistorius ameshinda katika mashindano ya olimpiki ya wasiojiweza 2012
Mwendesha mashtaka akasema hii ni kutokana na kuwa ukweli ni : "Ulimfyetulia Reeva risasi."
"Sio kweli," Pistorius akajibu, huku akibubujikwa kwa machozi na kuilazimu mahakama kusitisha vikao kwa muda.
Pistorius alisema yeye na Bi Steenkamp walibarizi jioni pamoja kabla ashutuke usingizini kutokana na kusikia sauti iliyotoka bafuni.
Mashahidi wa upande wa mashtaka walieleza kusikia mwanamke aliyepiga kelele, lakini upande wa utetezi unakana ushahidi huo.
Iwapo Pistorius hatopatikana na hatia kwa mauaji, ni lazima mahakama ifikirie mashtaka mengine ya mauaji yalio au yasio na dhamira, ambayo Pistorius anaweza kuhukumiwa kifungo cha takriban miaka 15 gerezani.
Anakabiliwa na mashtaka ya kufyetua risasi mbele ya umma na kumiliki silaha kinyume cha sheria, mashtaka ambayo yote anaykana.
Hatama yake itaamuliwa na jaji anayesaidiwa na waangalizi wawili.
Oscar Pistorius anatambulika kwa umaarufu kama,"Blade Runner" kutokana na miguu bandia anayotumia kukimbilia.
Chanzo:BBC 
Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top