Unknown Unknown Author
Title: THRDC WAPINGA BUNGE KUPIGIA KURA MUUNDO WA SERIKARI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema hatua ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka kupiga kura kuamua muundo...
Olengurumwa -April8-2014 449e1
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema hatua ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka kupiga kura kuamua muundo wa serikali ni kosa kubwa la kisheria.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Onesmo Olengurumwa, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika warsha ya usalama na tathmini ya athari za kiusalama kwa waandishi wa habari.
Alisema suala la Muungano ni la wananchi na siyo la wajumbe 639, hivyo hawapaswi kuliamua kwa kupiga kura kwa kuwa wananchi wameshatoa maoni yao kwenye Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge hilo.
"Chombo cha kisheria, ambacho ni Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndicho kiliwahoji wananchi na hadi sasa hakuna chombo kingine kilichoeleza kuyakana maoni ya wananchi hao," alisema.
Olengurumo ambaye ni mwanasheria kitaaluma, alisema Bunge kupiga kura ya muundo wa serikali ni kosa kwa kuwa halina mamlaka ya kubadili na badala yake kufuata rasimu ya wananchi, ambayo ndiyo ya kuaminika siyo kuwaamulia.
"Kuna nchi, ambazo ziliruhusu mambo yenye utata kupelekwa kwa wananchi na kupigiwa kura ya maamuzi, suala la Muungano linaweza kusubiri kwanza na kupelekwa kwa wananchi kwa ajili ya maamuzi," alisema Olengurumwa.
Alisema wajumbe hao wasijisahau na kuamua mambo ambayo hawana mamlaka nayo kwa kuwa Muungano wa nchi mbili hauwezi kuamualiwa na watu 639.
Olengurumo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni tata kuliko yote duniani, hivyo unapaswa kuchukuliwa kwa umakini mkubwa.
CHANZO NIPASHE

MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top